METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, November 11, 2017

MHANDISI MTIGUMWE ATOA MWEZI MMOJA KWA MRATIBU OFISI YA UKAGUZI KANDA YA KASKAZINI KUBAINI WALA RUSHWA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe (Kushoto) akisalimiana na Mratibu wa Ofisi ya Ukaguzi Kanda ya Kaskazini Ndg Juma Mwinyimkuu mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza na wafanyakazi wa Ofisi ya Ukaguzi Kanda ya Kaskazini mara baada ya kuwasili kwa ziara ya kikazi.

Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Ofisi ya Ukaguzi Kanda ya Kaskazini kwa ziara ya kikazi.
Baadhi ya wafanyakazi Ofisi ya Ukaguzi Kanda ya Kaskazini-Arusha wakifatilia kikao cha kazi kilichoongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisisitiza jambo kwa njia ya simu kwa watumishi waliopo Mjini Dodoma kuongeza ufanisi katika kazi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe (Katikati), Mkurugenzi wa Idara ya Utafiti na Maendeleo Dkt. Hussein Mansoor (Kulia), Mratibu wa Ofisi ya Ukaguzi Kanda ya Kaskazini Ndg Juma Mwinyimkuu (Kushoto) na Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala wa Wizara ya Kilimo Bi Hilda Kinanga wakiwasili Ofisi ya Ukaguzi Kanda ya Kaskazini.


Na Mathias Canal, Arusha

Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Mhandisi Methew John Mtigumwe Ametoa mwezi mmoja kwa Mratibu Ofisi ya Ukaguzi Kanda ya Kaskazini Ndg Juma Mwinyimkuu Kufatilia na kuwabaini baadhi ya watumishi wanaochukua Rushwa.

Mhandisi Mtigumwe alitoa maelekezo hayo wakati alipotembelea Kituo huduma ya afya ya mimea kilichopo katika Kijiji cha Tengeru, Kata Patandi, Wilaya ya Arumeru, Mkoani Arusha

Kituo hicho kinajihusisha na Ukaguzi wa Mazao na Udhibiti wa ndege waharibifu, Viwavijeshi pamoja na huduma ya kutoa vyeti vya usafi (Phtosanitary Certificate).

Mhandisi Mtigunmwe alisema kuwa Rushwa imekuwa tatizo sugu katika kituo hicho hususani katika utoaji wa vibali vya usafirishaji wa chakula kinyume na taratibu.

Aliwaasa watumishi hao kuacha haraka Utendaji mbovu, kuacha kuchukua Rushwa kwenye mipaka ni lawama nyingi kutoka kwa wananchi kwani kufanya hivyo wanaichafua wizara nzima ya kilimo.

lakini pia hakuna maabara na hawajatoa taarifa kwa Katibu mkuu wa wizara ya kilimo

"Nakupa mwezi mmoja uwakamate watu wote wanaochukua rushwa pia uandike barua ya kunitaarifu kuwa kuna uhitaji wa maabara" Alisema Mhandisi Mtigumwe wakati wa kikao hicho

MWISHO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com