Mkuu wa
Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) akitoa
neno la ukaribisho kwa wadau wa sekta ya elimu wakati wa hafla ya
kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu
nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Katikati ni mgeni rasmi
Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa aliyemwakilisha Katibu
Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof. Sifuni Mchome. Kushoto
ni Ofisa wa Ubalozi wa China, LIU Yun.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog)
Na Mwandishi Wetu
SHIRIKA
la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), limekabidhi
rasmi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu
nchini kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Makabidhiano
hayo yamefanyika jana jijini Dar es salaam katika hafla iliyohudhuriwa
na wadau walioshiriki katika uandazi wa kitabu hicho, ikiwamo serikali
ya China.
Kitabu
hicho ni matokea ya mradi wa CFIT wa UNESCO na serikali ya China wenye
lengo la kusaidia Serikali ya Tanzania kuimarisha umahiri wa wakufunzi
na walimu kwa kuwawezesha kujua Tehama na kuitumia.
Mradi huo
umelenga kuongeza uwezo wa vyuo vya walimu na teknolojia ya kisasa ya
Tehama na vifaa vyake ili kusaidia kujifunza na kufunza.
Alisema lengo la mradi huo ni kuwezesha wanafunzi na walimu wao kuongeza maradufu uwezo wao katika elimu.
Mgeni
rasmi Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella Bhalalusesa akisoma hotuba ya
ufunguzi kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
Prof. Sifuni Mchome wakati wa hafla ya kukabidhiwa kitabu cha mafunzo ya
Tehama kwa wakufunzi wa vyuo vya ualimu nchini kwa ajili ya Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi kilichoandaliwa na mradi wa CFIT wa UNESCO na
serikali ya China.(P.T)
Akipokea
kitabu hicho kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi Prof. Sifuni Mchome, Kamishina wa Elimu, Profesa Eustella
Bhalalusesa ameishukuru UNESCO na serikali ya China ya kuwezesha
upitiaji wa kitabu hicho kinachotoa mwelekeo wa mafunzo ili kuambatana
na maagizo ya viwango yaliyotolewa na Shirika la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO),
Alisema kitabu hicho kinatoa mwelekeo wa utekelezaji wa elimu ya Tehama kwa kuzingatia uwezo na weledi katika ufundishaji.
Kamishina
huyo amesema kwamba kazi ya kuangalia viwango hivyo iliyofanywa
kutokana na Mfuko wa China na Unesco kwenye moduli sita za uelewa na
elimu ya teknolojia kwenye Tehama.
Alishukuru
timu iliyopitia viwango hivyo na kusema serikali ya Tanzania inashukuru
msaada huo wa Unesco na serikali ya China kwa kufanikisha kazi hiyo kwa
ufanisi mkubwa.
Ofisa wa
Ubalozi wa China, LIU Yun akitoa salamu za Balozi wa China nchini kwenye
hafla ya kukabidhi kitabu cha mafunzo ya Tehama kwa wakufunzi wa vyuo
vya ualimu na walimu nchini kwa ajili ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya
Ufundi.
Ni
matumaini yake kwamba sasa Tanzania ina kielelezo cha kufuatia katika
kufanikisha maandalizi ya walimu wenye weledi na uwezo katika kufundisha
na kutumia teknolojia ya Tehama.
Naye Mkuu
wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akizungumza
kabla ya kukabidhi kitabu hicho alisema UNESCO itaendelea kushirikiana
na serikali ya Tanzania katika kuimarisha elimu ya Tehama ili kufungua
njia pana zaidi ya maendeleo.
Aidha
ameikumbusha serikali ya Tanzania kutumia vyema kitabu hicho katika
kuhakikisha kwamba mafunzo ya kariba ya hali ya juu yanatolewa ili kuwa
na mafanikio makubwa katika sekta zote za elimu na teknolojia.
Alisema
kitabu hicho kinatoa mwelekeo wa hatua kwa hatua katika mafunzo ya
Tehama na namna ya kufanikisha katika kumwelimisha mwanafunzi na vitu
vinavyoweza kufanywa ili kuhakikisha kwamba elimu sahihi inawafikia
wahusika.
Naye
Balozi wa China nchini, Dk. Lu Youqing kupitia kwa Ofisa wa Ubalozi Liu
Yun aliyefika kwenye hafla hiyo, alisema kwamba serikali ya China
itaendelea kushirikiana na Tanzania katika kuboresha elimu ya Tehama
nchini.
Naye
Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT Kutoka UNESCO, Faith Shayo
alishawahi kusikika akisema utoaji wa mwongozo huo ni sehemu ya
maandalizi ya mafunzo na matumizi ya maabara katika vyuo vya Monduli na
Tabora katika kufunza Tehama ili kuboresha mafunzo na ufundishaji.
Ingawa
kwa sasa vyuo vinavyofanyiwa kazi na mradi huo vipo viwili vya Tabora na
Monduli vipo vingine vinane vinavyofunza walimu wa sayansi na hesabu
ambavyo vitaingizwa katika mradi.
Mratibu
wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo akielezea
maandalizi na hatua walizopitia katika uandaaji wa kitabu hicho mpaka
kukamilika kwa wadau wa sekta ya elimu walioshiriki hafla hiyo.
Meza kuu ikimpongeza Mratibu wa kitaifa wa Mradi wa CFIT kutoka UNESCO, Faith Shayo (hayupo pichani).
0 comments:
Post a Comment