Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe,
akizungumza na Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa
nchini, kuhusu nafasi na majukumu yao katika uchaguzi mkuu, pamoja na
jinsi Serikali ilivyojipanga kuhakikisha uchaguzi unakuwa wa amani, huru
na haki kwa vyama vyote.
Waheshimiwa
Mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini,
wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mhe. Bernard Membe, wakati wa mkutano huo uliofanyika jana
10-09-2015 katika ukumbi wa mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius
Nyerere (JNIC) jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
na Mkuu wa Itifaki, Balozi Mohammed Maharage Juma, akiwatambulisha
Mabalozi waliowasili nchini hivi karibuni ambao ni mara yao ya kwanza
kuhudhuria Kikao cha aina hii, Wizara ya Mambo ya Nje.
Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini Mhe.Thamsanga Dennis Mseleku akiuliza swali katika mkutano huo.(P.T)
Balozi wa Umoja wa Ulaya Mhe. Filiberto Sebregondi, akiuliza swali katika mkutano huo.
Waziri wa
Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe, akijibu
Maswali ya Waheshimiwa Mabalozi. Kushoto kwake ni Balozi wa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo na Mkuu wa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa
nchini Mhe. Juma Khalifan Mpango. Kulia kwake ni Naibu Waziri Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim na Katibu
Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi,
Liberata Mulamula.
Picha ya pamoja.
Picha: Reuben Mchome/Blogu ya Wizara
0 comments:
Post a Comment