Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya HORTI Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti
Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI Tengeru) wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Methew John Mtigumwe
wakati wa kikao cha kazi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe akiwasili katika Ofisi za Taasisi ya
Horti
Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI Tengeru). Mwingine ni
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt Mansoor Hussein
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Taasisi ya Horti
Tengeru na Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti
Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI-Tengeru) wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe
wakati wa kikao cha kazi
Afisa Mfawidhi -HORTI-Tengeru akisoma Risala kwa niaba ya watumishi wenzanke wakati wa kikao cha pamoja na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe
wakati wa kikao cha kazi.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya HORTI Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (Horti
Tengeru) wakimsikiliza Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe
wakati wa kikao cha kazi.
Afisa Mkuu wa Utafiti wa Kilimo Bi Alice M. Kavishe akichangia mada wakati wa kikao cha pamoja na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe
wakati wa kikao cha kazi.
Afisa Mkuu wa Utafiti wa Kilimo Dkt Stephen Sebastian Kuoko akichangia mada wakati wa kikao cha pamoja na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe
wakati wa kikao cha kazi
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe
akizungumza wakati wa kikao cha kazi na watumishi wa Taasisi ya Horti
Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI Tengeru).
Baadhi ya watumishi wa Taasisi ya Horti
Tengeru na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mboga Matunda na Maua (HORTI Tengeru) wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John Mtigumwe
wakati wa kikao cha kazi.
Na Mathias Canal, Arusha
Serikali
imekuwa ikiongeza idadi ya wanafunzi katika Vyuo vya Kilimo na kwa sababu hiyo
Maafisa Ugani wamekuwa wakiongezeka kila mwaka ambapo hali hiyo imewezesha Karibu
kila Kata hapa nchini kuwa na Afisa Ugani.
Lakini
pamoja na kuwepo kwa wataalamu hao wa kilimo bado uzalishaji wa mazao
mbalimbali nchini yakiwemo mazao ya chakula na biashara si wa kuridhisha ambapo
wakulima wanalima na kupanda pasina hata kufuata hatua za kitaalamu.
Hayo
yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo nchini Mhandisi Mathew John
Mtigumwe wakati wa kikao cha kazi akizungumza na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo
ya Mboga Matunda na Maua (HORTI TENGERU) kilichopo katika Kijiji cha Tengeru, Kata Patandi, Wilaya ya Arumeru Mkoani
Arusha.
Alisema lengo la Serikali
kusambaza Maafisa Ugani kwenye Halmashauri mbali mbali nchini ilikuwa kuwasaidia wakulima waweze
kufanya Kilimo kwa Ufanisi na kuongeza mavuno.
Hata
hivyo jambo hilo limekuwa kinyume kwani asilimia kubwa ya maafisa ugani ama
hawafanyi kazi zao ipasavyo ama wameshindwa kusimamia majukumu yao ipasavyo.
Mhandisi
Mtigumwe alisema kuwa Wizara ya kilimo inaandaa utaratibu wa kuwarudisha shule
maafisa ugani wasiofaa kutokana na uchache wa
ellimu zao na uwajibikaji huku wale ambao watashindwa kabisa kuwa msaada kwa
wakulima baada ya masomo wizara itapendekeza waondolewe kazini.
Alisema Maafisa ugani hao
Watafanyiwa usaili upya ili kubaini uwezo wao kwani wengi wao wameajiriwa na
serikali lakini wakulima hawanufaiki na kilimo tafsiri yake Wataalamu hao ama hawatekelezi
wajibu wao au hawana uwezo wa kutekeleza ipasavyo.
Aidha,
alisema Maafisa ugani kote nchini wanatakiwa kuwekeza kwenye utoaji wa
Huduma ya Ugani kwa Wakulima ili iwe rahisi kwa Mkulima
kusaidika katika uzalishaji wa mazao mbalimbali ya biashara na kilimo.
Sambamba na hayo pia aliwasihi Wakufunzi
katika chuo hicho kujiendeleza kielimu huku akisema kuwa Wizara ya kilimo lazima
itengeneze mpango wa kuwaendeleza wakufunzi ili kuzalisha wataalamu wenye
ufanisi zaidi.
Alisema anatambua kuwa Mahitaji ni
makubwa katika vyuo vya kilimo hivyo Wizara inatazama namna ya kuongeza chuo
kingine kama hicho huku akiwasisitiza wataalamu hao kubadili mfumo badala ya
kusoma kwa jumla masomo mengi na kufikia hatua ya kuchagua eneo maalumu la
kusoma (Kozi) kwani Kilimo ni somo pana.
“Nategemea muandae mpango maalumu
ambao utapelekea Kuwa na kozi za muda mchache sio lazima kuwa na kozi za muda
mrefu pekee kama ilivyo hivi sasa” Alisema Mhandisi Mtigumwe
Katika hatua nyingine amewataka Watumishi
wote kuongeza spidi katika utendaji wa kazi ili kuunga mkono juhudi za Mhe Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na serikali ya awamu
ya tano yenye kauli mbiu ya HapaKaziTu.
Sambamba na kutembelea na kuzungumza
na watumishi na wakufunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Mbogamatunda na Maua (HORTI
TENGERU) Akiwa ziarani Mkoani Arusha Katibu Mkuu Mhandisi Methew Mtigumwe
alitembelea pia Taasisi ya Utafiti Horti Tengeru, Taasisi ya Utafiti wa Kilimo
na Maendeleo Kanda ya Kaskazini (NZARDI) na Taasisi ya Utafiti ya kudhibiti
visumbufu katika Ukanda wa Tropiki.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment