Picha ya pamoja kati ya Mkuu wa Mkoa
Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (wa pili kushoto) na Balozi wa China Mheshimiwa
Wang Ke (wa pili kulia) mara baada ya kumalizika mazungumzo yao, kushoto ni
Katibu Tawala Mkoa Dodoma Ndg. Rehema Madenge na kulia ni Afisa kutoka Ubalozi
wa China.
Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Dodoma Makao Makuu
Balozi wa China hapa nchini Mhe.Wang
Ke ameahidi Serikali yake itatoa msaada wa kugharamia mradi wa uchimbaji kisima
kimoja cha maji na miundombinu ya usambazaji wa huduma hiyo kwenye moja ya
kijiji cha Mkoa wa Dodoma.
Balozi Wang Ke alimuahidi msaada huo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge leo alipomtembelea na kufanya nae
mazungumzo Ofisini kwake Mjini Dodoma, ambapo alimtaka Dkt. Mahenge kutumia
timu ya Watalaalamu wa Maji wa Mkoa kufanya usanifu na makadirio ya bajeti ya
mradi huo na kuiwasilisha Ofisi za Ubalozi wa China kwa ajili ya kuanza
utekelezaji wa mradi.
Aidha, Balozi Wang Ke ameelezea kuwa
Uongozi wa Mkoa utaainisha ni kijiji kipi ambacho kitapewa fursa ya kupatiwa
mradi huo.
Kwa upande wake, Dk. Mahenge
ameishukuru Serikali ya China kupitia kwa Balozi Wang Ke kwa ajili ya mradi huo
na amebainisha kuwa mradi huo pia unaweza ukatumika kuwasaidia vijana kwenye
kijiji kitachopewa mradi kuanzisha mradi wa kilimo cha umwagiliaji.
Dkt. Mahenge amemwelezea Balozi Wang
Ke kuwa amefanya ziara kwenye Wilaya za Mkoa wa Dodoma na amejionea namna
ambavyo wananchi wanahitaji kubwa la maji na hivyo mradi huo umekuja wakati
muafaka kabisa.
Katika mazungumzo ya Viongozi hao,
mradi huo utahusisha Utafiti wa uwezekano wa kupata maji chini ya Ardhi,
Uchimbaji wa Kisima kirefu, ununuzi wa mashine ya kuvuta na kusukumia maji,
ujenzi wa Miundombinu ya kusambazia maji, Tenki la kuhifadhia maji na vituo vya
wananchi kuchotea maji.
0 comments:
Post a Comment