METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, October 14, 2017

Wakamba wamtaka Kalonzo ajiondoe upinzani

 
Kikundi cha viongozi wa Ukambani kimeitaka jumuiya hiyo kuachana na upinzani na badala yake wamuunge mkono Rais Uhuru Kenyatta.
Wakizungumza katika nyakati tofauti kwenye kaunti za Machakos na Makueni wakati wa msafara wa wapigadebe wanaojiita Uhuru Express, wazee wa baraza la uongozi wa jamii ya Wakamba na kikundi cha washirika wa Jubilee wametoa wito kwa kiongozi wa chama cha Wiper ambaye ni mshirika wa Nasa Kalonzo Musyoka kuungana na chama tawala.
Wazee hao wakiongozwa na mwenyekiti wao Boniface Kilonzo walizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Machakos ambako mwenyekiti wa zamani wa Bodi ya Chuo cha Mafunzo ya Madaktari, Philip Kaloki aliwaalika wanasiasa katika kikao cha Kambu, Kibwezi Mashariki
Kilonzo alimsihi kiongozi wa muungano wa upinzani (Nasa) Raila Odinga kusitisha maandamano anayotaka yafanyike nchi nzima akisema yanachochea ghasia.
“Maandamano haya hayafanyiki kwa nia njema kwa sababu yanalenga kuzua vurugu na uharibifu wa mali. Huu ni uhujumu uchumi na unaoweza kuadhibiwa kisheria,” alisema.
Pia alisema uamuzi wa Raila kujiondoa kushiriki kwenye uchaguzi wa marudio wa Oktoba 26 hauna nia njema. “Njia pekee ya kufikia uongozi katika nchi yetu ni kupitia sanduku la kura. Kujiondoa kwa Raila kushiriki uchaguzi ni ishara kwamba ushiriki wao ulikuwa wa kibinafsi na si kwa masilahi ya Wakenya,” aliongeza.
Viongozi hao walisema jamii yao inapoteza mengi kwa kusimama na upinzani. Mbunge wa zamani Kisoi Munyao alisema ushirika wa Kalonzo na Raila haubebeki tena na ni hasara kwa jamii ya Wakamba.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com