Wakazi wa Kata ya Rau Mitaa ya
Kariwa Chini, Kalikacha na Sabasaba wakipata huduma ya kujaziwa fomu za
maombi ya Vitambulisho vya Taifa. Zoezi katika Kata hiyo linafanyika
katika shule ya msingi Rau Wilaya ya Moshi – Kilimanjaro.
Wananchi katika Kata ya Ng’ambo
Mitaa ya Mnazi, Lombeta na Ng’ambo wakiwa katika harakati za kukamilisha
fomu zao, kuhakikiwa na Idara ya Uhamiaji na kugongewa mihuri na
watendaji kwenye mitaa yao kabla ya kuingia kwenye chumba maalumu
kupigwa picha na kuchukuliwa alama za vidole na saini .
………………..
Wananchi katika Kata za Ng’ambo,
Rau na Mfumuni wameendelea kujitokeza kwa wingi kusajiliwa Vitambulisho
vya Taifa katika zoezi linaloendelea kwa sasa katika mkoa wa Kilimanjaro
huku wananchi wakihimizana na kuhamasishana kwa njia ya ujumbe mfupi
sms na simu.
Diwani wa Kaya ya Ng’ambo Mhe.
Genesis Seth Kiwelu (Chadema) amesema wananchi wa Kata ya Ng’ambo
wamebuni utaratibu mzuri wa kuhakikisha wanapeana taarifa ya kuwepo
kwenye vituo vya usajili kwa siku ambazo zimepangwa; na kutoa kipaumbele
kwa wazee na wasio jiweza pindi wanapofika kusajiliwa.
“ Kata ya Ng’ambo ina wananchi
wengi na tunafanya jitihada za kuhakikisha wananchi wote wenye miaka 18
wanasajiliwa na tumebuni mbinu ya wananchi kuhamasishana kwa njia
mbalimbali” alisema
Zoezi la Usajili kwa Wilaya ya
Moshi kwa Kata za Ng’ambo, Rau na Mfumuni linamalizika Ijumaa 20/10/2017
na litaendelea kwa Kata za Msaranga, Miembeni na Majengo.
Afisa Usajili Mkoa wa Kilimanjaro
Bw. Brighton Mtugani amewataka wananchi katika Kata zinazofuata kuanza
kuandaa nyaraka zao muhimu zitakazowatambulisha ili zoezi hilo kwenye
kwa haraka na kwa muda uliopangwa.
Viambatisho ambavyo mwananchi
anatakiwa kuwa navyo ni pamoja na Cheti cha kuzaliwa, Vyeti vya Shule,
Pasi ya kusafiria(Passport), Kati ya Kupigia Kura, Leseni ya Udereva,
Nambari ya Utambulisho ya Mlipa Kodi (TIN),Kitambulisho vya Mzanzibari
Mkaazi, Kadi ya Bima ya Afya na Kadi ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii.
Wilaya zingine zinazoendelea na
zoezi hilo kwa Mkoa wa Kilimanjaro ni Same Kata za Same, Kisima na
Njoro, Mwanga Kata za Mwanga, Kileo na Lembeni. Wilaya zingine ni Rombo,
Siha na Hai
0 comments:
Post a Comment