Mkufunzi kutoka kampuni ya Cornerstone,David Christian, akibadilishana mawazo na baadhi ya wafanyakazi wa TDL
Baadhi
ya wafanyakazi wa TDL wakimsikiliza kwa makini mtaalamu wa masuala ya
fedha kutoka kampuni ya Cornerstone.Elvis Kato,wakati wa mafunzo hayo
Baadhi ya wafanyakazi wa TDL wakifuatilia mafunzo kutoka kwa wakufunzi
……………..
Kampuni ya Tanzania Distillers Limited (TDL) iliyopo chini ya kampuni mama ya TBL Group imewezesha wafanyakazi wake kupata mafunzo ya mbinu za biashara na matumizi mazuri ya
fedha ambayo yametolewa na wataalamu kutoka kampuni ya masuala la
ushauri na mafunzo ya biashara ya Cornerstone Partners ya jijini Dar es
Salaam.
Mafunzo hayo ya wafanyakazi ni mwendelezo wa mkakati wa kampuni ya TBL Group wa kuwapatia wafanyakazi wake mafunzo mbalimbali ya
nje na ndani ya kampuni lengo kubwa likiwa ni kuwawezeha kupata ujuzi
wa kufanya kazi zao kwa ufanisi sambamba na maarifa ya kukabiliana na
changamoto mbalimbali katika maisha yao ya kila siku.
Masuala
ambayo walifundishwa ni kuhusiana na mipango ya matumizi ya fedha,jinsi
ya kujiwekea akiba na kufanya uwekezaji wenye tija,kupanga kuendeleza
taaluma zao,ujasiriamali na jinsi ya kulinda mali walizonazo zisipotee bila mpangilio.
Wakiongea
baada ya kumalizika mafunzo,baadhi ya wafanyakazi walishukuru mwajiri
wao kwa kuwaandalia mafunzo ya mara kwa mara ya kuwajenga na kuwasaidia
katika maisha yao ya kila siku kama ambavyo wamepata mbinu mbalimbali
kuhusiana na matumzi mazuri ya fedha ,uwekezaji na ujasiriamali.
0 comments:
Post a Comment