Tume ya mawasiliano nchini Uganda (UCC) imepiga marufuku kwa vyombo vya
habari nchini humo kufanya 'interview' na mwanamuziki Bobi Wine, baada
ya kuonekana kinara kwenye suala la kupinga ukomo wa urais nchini humo.
Taarifa
hiyo imetolewa na mwenyewe Bobi Wine ambaye pia ni mbunge wa upinzani
nchini humo kwenye ukurasa wake wa instagram akisema kuwa amepigiwa simu
na baadhi ya vyombo vya habari nchini humo na kuthibitisha suala hilo,
kuwa wamepigwa marufuku kufanya naye mahojiano yoyote.
"Hii asubuhi nilitakiwa kufanya mahojiano na Capital FM, baadaye
nikataarifiwa kuwa wamepewa agizo na UCC na kupigiwa simu na watu wa
usalama kwamba wasiwe na mimi, nikapigiwa simu na vituo vingine vya
redio na runinga na kunithibitishia wamepewa agizo hilo hilo na kwa
vitisho, na iwapo watakuwa na mimi watakuwa katika hatari ya kufungiwa",
ameandika Bobi Wine.
Bobi Wine ameendelea kuandika akisema kwamba.. "Iwapo unaangalia
dalili za kuanguka kwa serikali usiendelee tena, huu ni upumbavu na
haukubaliki, serikali inadhani inaweza kutuzuia kufikia watu wetu,
wanafanya vitu ambavyo havina tofauti na vile wanavyohubiri kuvipinga",
Bobi WIne amekuwa miongoni mwa viongozi maarufu ambao wanapinga
vikali suala la kutaka kupitishwa kwa katiba ambayo itongeza muda wa
ukomo wa urais, kitendo ambacho kitamruhusu Rais Yoweri Museveni wa nchi
hiyo, kugombea tena awamu ijayo.
0 comments:
Post a Comment