Na: Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA
Watanzania waaswa kuwa wabunifu katika kutengeneza mifumo itakayosaidia uboreshaji na utoaji huduma kwa jamii.
Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Wilaya
(DMO) wa Halmashauri ya Mbulu Mkoa wa Manyara Dkt. Joseph Fwoma wakati
wa Mafunzo ya Mfumo wa Kielekroniki (PlanRep) iliyorekebishwa wa kuandaa
Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa
yanayoratibiwa na Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma(PS3) kwa
kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID)
leo Mjini Dodoma.
Dkt.Fwoma amesema kuwa Mfumo huo
umeundwa na kusukwa na watanzania wenyewe kwa lengo la kushirikiana na
Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za Serikali za Mitaa kea
jamii hasa katika kuandaa Mioango, Bajeti na Ripoti za Serikali.
Aidha, Dkt. Fwoma amesema kuwa Mfumo huo
utasaidia kupunguza muda, gharama na kuboresha utendaji kazi katika
uandaaji wa Mipangi na Bajeti za Serikali kwa watumishi wa Serikali
endapo kika mtumishi atatimiza wajibu wake.
“Mfumo uliokuwa ukitumika awali ulifanya
baadhi ya watumishi kudanganya baadhi ya takwimu na hata taarifa
mbalimbali pindi zinapohitajika, hivyo kupitia mfumo huu hatutegemei
kupata taarifa za udanganyifu” ameeleza Dkt. Fwoma.
Kwa upande wake Mganga Mku wa
Wilaya(DMO) wa Halmashauri ya Singida Dkt. Sungwa Kabisi amesema kuwa
mfumo uliokuwa ukitumika awali ulishirikisha watendaji wachache na hivyo
kupel3kea baadhi ya mapungufu katika utendaji kazi.
“Mfumo umerahisisha utendaji kazi ambapo
kila mhusika anauwezo wa kuwakisilisha majukumu yake, umeruhusu
masahihisho na pia kila mtumishi anauwezo wa kujipima kulingana na
utendaji kazi wake” ameongeza Dkt.Kabisi.
Mfumo wa Kielektroniki (PlanRep)
iloyoboreshwa upo chini ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo wa Sekta za
Umma(PS3) ikiwa ni mradi wa miaka mitano ulioanza mnamo Julai 2015 na
kutarajiwa kukamilika Julai 2020 ambapo utarahisisha utendaji kazi na
kusaidia kutatua changamoto zilizokuwepo awali.
0 comments:
Post a Comment