Msajili wa Kitengo cha Hati; Bwn. Kastor Ngonyani akizungumzia Maboresho yaliyofanyika katika ofisi yake.
Afisa katika Kitengo cha Hati akimhudumia mteja aliyefika katika dawati lake.
Maafisa mbalimbali katika Kitengo cha
Hati. Na wengine wa Idara mbalimbali za Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi wakiendelea kuhudumia Wananchi katika Kituo cha
Huduma kwa Mteja Wizarani hapo.
Maafisa mbalimbali katika Kitengo cha
Hati. Na wengine wa Idara mbalimbali za Wizara ya Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi wakiendelea kuhudumia Wananchi katika Kituo cha
Huduma kwa Mteja Wizarani hapo.
……………………………………………………………………………….
Kitengo cha Usajili wa Hati na Nyaraka
katika Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kimefanya
maboresho katika upatikanaji wa Hati na Nyaraka kwa muda mfupi zaidi na
ilivyokuwa hapo awali.
Akizungumza wizarani hivi karibuni;
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Hati; Bwn. Kastor Ngonyani alisema; Katika
zoezi la usajili wa Hati mpya zilizokuwa zikiandaliwa kwa muda wa miezi
mitatu toka tarehe ya kuwasilishwa kwa Msajili, sasa zoezi hilo
linachukua wiki mbili tu. Ameeleza utaratibu huo umerahisishwa kwa
kutumia mfumo wa Kielektroniki.
Aidha, Bwn. Ngonyani alisema kwa nyaraka
nyingine zinazohusu Ardhi, kama zile za Uhamisho, Mikopo na zile
zisizohusu Ardhi/za mali zinazohamishika zinatumia wiki moja tu kuwa
tayari kutoka tarehe ambapo nyaraka husika iliwasilishwa kwa Msajili wa
Hati.
Vile vile, Msajili alisema kwamba utoaji
wa taarifa nyingine za upekuzi/ Search ambazo huhusisha taarifa
mbalimbali kama vile; Kujua kiwanja ni cha matumizi gani, kina Hati au
hakina, Mmiliki wake ni nani na taarifa zinazofanana na hizo kuhusu
Historia ya kiwanja husika; ” Sasa taarifa hizo zinapatikana kwa siku
mbili tu, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo zoezi hilo lilikuwa
linachukua wiki mbili, mwezi mzima au hata zaidi,” alisema Bwn.
Ngonyani.
Bwn. Ngonyani alieleza jinsi ambavyo
ofisi yake imekuwa na Hati na nyaraka mbalimbali za Wananchi ambao bado
hawajafika kuchukua Hati na Nyaraka hizo, licha ya nyaraka hizo kuwa
tayari kwa muda mrefu uliopita. Bwn. Ngonyani alitoa rai kwa Wananchi
wote ambao walishafika katika ofisi yake kwa ajili ya kupatiwa huduma
hizo wafike kuchukua Hati na Nyaraka hizo muhimu kwao.
Ofisi ya Kitengo cha Msajili wa Hati ipo
kisheria . Sheria zinazoainisha uwepo wake sambamba na majukumu yake
ni ; Sheria ya Usajili wa Ardhi , Sura ya 334 ya Sheria za Nchi; Sheria
ya Usajili wa Nyaraka, Sura 117 ya Sheria za Nchi; Sheria ya Uhamisho
wa Mali/Usajili wa Mali zinazohamishika, Sura 210 ya Sheria za Nchi na
Sheria za Usajili wa Majengo ( Unit Tittle Act).
0 comments:
Post a Comment