Sunday, September 3, 2017

WATANZANIA WAASWA KUWA WABUNIFU

27. Mganga Mkuu wilaya ya Singida Vijijini, Dkt Erick Bakuza JPG
Na: Beatrice Lyimo- MAELEZO, DODOMA

Watanzania waaswa kuwa wabunifu katika kutengeneza mifumo itakayosaidia uboreshaji na utoaji huduma kwa jamii.

Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Wilaya (DMO) wa Halmashauri ya Mbulu Mkoa wa Manyara Dkt. Joseph Fwoma wakati wa Mafunzo ya Mfumo wa Kielekroniki (PlanRep) iliyorekebishwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa yanayoratibiwa na Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma(PS3) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) leo Mjini Dodoma.

Dkt.Fwoma amesema kuwa Mfumo huo umeundwa na kusukwa na watanzania wenyewe kwa lengo la kushirikiana na Serikali katika kuboresha utoaji wa huduma za Serikali za Mitaa kea jamii hasa katika kuandaa Mioango, Bajeti na Ripoti za Serikali.

Aidha, Dkt. Fwoma amesema kuwa Mfumo huo utasaidia kupunguza muda, gharama na kuboresha utendaji kazi katika uandaaji wa Mipangi na Bajeti za Serikali kwa watumishi wa Serikali endapo kika mtumishi atatimiza wajibu wake.

“Mfumo uliokuwa ukitumika awali ulifanya baadhi ya watumishi kudanganya baadhi ya takwimu na hata taarifa mbalimbali pindi zinapohitajika, hivyo kupitia mfumo huu hatutegemei kupata taarifa za udanganyifu” ameeleza Dkt. Fwoma.

Kwa upande wake Mganga Mku wa Wilaya(DMO) wa Halmashauri ya Singida Dkt. Sungwa Kabisi amesema kuwa mfumo uliokuwa ukitumika awali ulishirikisha watendaji wachache na hivyo kupel3kea baadhi ya mapungufu katika utendaji kazi.

“Mfumo umerahisisha utendaji kazi ambapo kila mhusika anauwezo wa kuwakisilisha majukumu yake, umeruhusu masahihisho na pia kila mtumishi anauwezo wa kujipima kulingana na utendaji kazi wake” ameongeza Dkt.Kabisi.

Mfumo wa Kielektroniki (PlanRep) iloyoboreshwa upo chini ya Mradi wa Uimarishaji Mifumo wa Sekta za Umma(PS3) ikiwa ni mradi wa miaka mitano ulioanza mnamo Julai 2015 na kutarajiwa kukamilika Julai 2020 ambapo utarahisisha utendaji kazi na kusaidia kutatua changamoto zilizokuwepo awali.

No comments:

Post a Comment