Mkuu wa wilaya wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo
Na Mwamvua Mwinyi,Rufiji
Jumla ya wanafunzi
wa kike nane wa shule za sekondari na saba wa shule za msingi wilayani
Rufiji mkoani Pwani ,wamebainika kuwa wana mimba ,mwaka huu .
Kutokana na taarifa
hiyo ,mkuu wa wilaya ya Rufiji ,Juma Njwayo ,amewaasa wanafunzi wa kike
kuacha kukimbilia mambo ya ovyo badala yake wajidhatiti katika elimu ili
kupata maarifa na ufahamu .
Akizungumza baada ya
kukamilisha ziara yake ya mwezi mmoja ,ya kutembelea shule 43
,kuzungumza na wazazi na walezi ,alisema mimba za utotoni zinakwamisha
jitihada za kumkomboa mtoto wa kike kitaaluma.
Njwayo alieleza
,kati ya mimba zilizobainika mwanafunzi mmoja ni wa shule ya sekondari
Ngorongo ,Nambunju saba na wengine saba ni wa shule za msingi.
Alifafanua ,zipo
hatua za kisheria zinazochukuliwa kwa waliohusishwa kuwatia mimba
wanafunzi hao,; ambapo watendaji wa kata wameshawashtaki kwenye vyombo
vya sheria .
Alisema ,pia
wanatengeneza mazingira mazuri kwa watoto mashuleni kwa kuwataka walimu
wakae nao mara kwa mara kuwaelimisha wajiepushe na wanaume wadanganyifu .
Kwa mujibu wa Njwayo
,kilichomsukuma kufanya ziara hiyo ilikuwa baada ya kupata taarifa kuwa
kuna wanafunzi watoro wa kudumu 190 kati ya wanafunzi 2,442
wanaotarajiwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu .
Aidha katika ziara hiyo amefanikiwa kuwarejesha
shule wanafunzi hao 54 wa shule ya Ikwiriri ,shule ya msingi Utete tisa
na shule ya msingi Mapinduzi tisa.
Njwayo
alielezea,alichogundua ipo changamoto ya wazazi kutokuwa na ushirikiano
na walimu na kutofuatilia mwenendo wa watoto wao kila siku .
“Elimu ni muhimu ,ni
nguzo na msingi wa maisha yetu ,na kwa watoto wetu ,itaweza kuwasaidia
kupata ufahamu wa kujiajiri na kuwa mwanakilimo bora wa kisasa na kuwa
na upeo kuliko kukosa elimu ” alisisitiza Njwayo.
Njwayo ,alisema
kwasasa kuna watendaji wa vijiji na kata wamefukuzwa kutokana na kukatwa
kwani hawakuwa na cheti cha kidato cha nne hivyo wanaajiriwa wapya
kuziba mapengo .
“Hapo ndipo inapoonekana thamani ya elimu ,hivyo wanafunzi waache michezo na vishawishi ,;wasome kwa bidii ” alisema Njwayo.
0 comments:
Post a Comment