Mmoja kati ya kundi kubwa la ng’ombe akishushwa baada ya
kuwasili katika eneo la kuchinja mapema leo tayari kwa kuchinjwa.
Waislamu duniani kote wanasherehekea sikukuu ya Idi ambayo husherehekewa
kwa kutoa sadaka ya kuchinja. Ngombe takriban 600 wanatarajiwa
kuchinjwa katika kipindi cha siku nne.
Kundi la ng’ombe wakiwa wamelazwa chini tayari kwa kuchinjwa
katika sikukuu ya Idi inayosherehekewa duniani kote na waumini wa dini
ya Kiislamu, siku hii ni siku maalumu ya kuchinja na kutoa sadaka.
Ng’ombe zaidi ya 600 watachinjwa mpaka kufikia kilele cha maadhimisho ya
sikukuu hiyo. Tukio la kuchinja limefanyika jijini Dar es Salaam katika
shule ya Feza Boys iliyoko Kunduchi.
Tukio la kuchinja likiambatana na dua linaendelea
Waandaaji wa nyama iliyochinjwa katika siku ya kuchinja ambayo
ni sikukuu ya Idi ambayo pia huambatana na hija. Waislamu duniani kote
leo wanasherehekea Sikukuu ya Idi.
Wasimamizi wa kugawa nyama
iliyojinjwa kama sadaka leo katika kituo cha shule ya Feza Boys iliyoko
Kunduchi, Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Tukio hilo hufanyika
kila mwaka katika kuadhimisha sikukuu ya Idi. Ng’ombe hukusanywa kutoka
kwa wafugaji mbalimbali nchini kwaajili ya kukamilisha tukio la
kuchinja ili kutoa sadaka.
PICHA ZOTE NA BLOG YA IMMA MATUKIO
KAWAIDA
0 comments:
Post a Comment