Mufti
Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakary Zubeiry bin Ally amesema pesa za
mahujaji wote walioshindwa kwenda katika ibada ya Hijja zitarejeshwa
ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo.
Sheikh
Zubeiry ameyasema hayo katika Baraza la Eid Al Adh’ha na kuwa amefanya
uamuzi huo baada ya baadhi ya mahujaji kushindwa kwenda Hijja kutokana
na taasisi zilizoandaa safari yao kushindwa kumamilisha taratibu zote
zinazohitajika.
Sheikh
Zubeiry amesema ataunda kamati maalumu ambayo itakuwa ikizifuatilia
taasisi ambazo zinahusika na kusafirisha mahujaji kwenda katika ibada ya
Hijja ambayo inafanyika katika mji wa Makkah na Madina.
“Nimekutana
na wawakilishi wa taasisi hizo mara mbili na tumekubaliana kuwa pesa
hizo zitarusishwa na zitatumika kufanya maandalizi kwa Hijja nyingine
labda hii haikuwa bahati yao lakini Hijja ijayo watakwenda,” alisema
Sheikh Zubeiry.
Kwa
upande wa mgeni rasmi katika Baraza la Eid,Waziri wa Ulinzi, Dkt.
Hussein Mwinyi aliwataka Watanzania kudumisha amani iliyopo nchini na
kuishi kwa upendo bila kubaguana kwa itikadi za kidini au kikabila.
0 comments:
Post a Comment