Moja
ya changamoto kubwa inayowakabili watu wengi ni kutojua kwa undani kipi
kipaji chako ambacho Mungu amekupa na ambacho unaweza ukakitumia kwa
namna moja ama nyingine ili uweze kuleta mabadiliko chanya katika jamii
na wewe binafsi.
Na
kwa kuwa kuna watu wengi ndio wapo kundi hilo, kuna usemi unasema ya
kwamba wengi wape basi ngoja nifanye hivyo kuweza kuwapa somo hilo la
namna ya kujua kipaji chako kwani hii itamsadia kila mmoja ambaye
atakwenda kufuatana nami mwanzo hadi mwisho katika mukutadha wa makala
haya.
Tunapozungumzia
neno kipaji huenda kila mmoja akawa na maana yake ambayo anaifahamu,
lakini kwa namna moja ama nyingine ni lazima mtu aweze kuzaliwa nacho
hivyo Mwenyezi Mungu huhusika pia katika kumpa mtu kipaji.
Hivyo
endapo mtu atakifahamu kipaji chake inampasa sasa ajue namna ya
kukiendeleza kipaji hicho ili kisife. Pia ikumbukwe ya kwamba
tunapozungumzia kipaji tunamzungumzia binadamu na maisha yake kwa
ujumla.
Katika
tafiti ambazo zimewahi fanywa na Dr. Fred Luskin kutoka Stanford
university yeye aliweza kugundua ya kwamba asilimia 65 ya watu wengi
hawajui vipaji vyao na katika kundi kubwa la idadi hii ya watu ndio
ambao wanafanya vitu ambavyo sio vyao.
Na
pia asilimia 35 iliyobaki hawa ndio ambao wameweza kuvijua hivyo
vipaji vyao ingawa haviwasadii katika maisha yao na wengine kwa asilimia
100, hii ni kutoka mafanikio yatokanayo vipaji hivyo huwa ni ya muda
mrefu.
Hivyo
kwa kuwa watu wengi tunataka mafanikio ya muda mfupi uvumilivu hufika
ukomo na kujikuta tunaviacha vitu hivyo na kuingia kufanya vitu vingine.
Mfano
mtu anakuwa na kipaji cha kucheza mpira katika timu kubwa hapa nchini
na nje ya nchi,na kwa kuwa huenda amecheza kwa muda mrefu bila matarajio
yake kutimia mtu huyo huacha kile ambacho hukifanya na kuamua kufanya
kitu kingine ambacho sio kipaji chake mwishowe mtu huyo anajikuta
anafanya hiki anakiacha mara kile nacho anakiacha.
Ukiona hicho unachokiita kipaji chako hakitoi burudani, hakifundishi, hakishangazi basi hicho sio kipaji.
Namna ya kugundua kipaji chako.
1. Kumuomba Mungu.
Hapa
huwa pananifanya nimkumbuke sana rafiki yangu Samweli Salali kwani
aliwahi kuniambia ya kwamba kipaji ni kusudio la Mungu kwa kila mja
wake. Kwani katika mafundisho yake katika vitabu vya dini vinasema kabla
sijaumba nilikujua.
Hii
inamaana kila mwanadamu aliyeumbwa na Mungu ana kipaji chake, hivyo
kinauwezo mkubwa wa kubadili maisha yake na jamii kwa ujumla, ila kipaji
hicho watu wengi hawahujui mpaka dakika hii kuwa kipi kipaji chake
ambacho Mungu kampa.
Hivyo
kama wewe ni miongoni mwa watu hao ni muda wako muafaka wa kutumia Muda
huu kumuomba Mungu akuonyeshe kipaji chako hasa na kipi kwa sasa?
2. Marafiki, ndugu na wazazi.
Hili
ni kundi muhimu sana ambalo litakusaidia wewe kujua kipaji chako. Labda
unaweza ukajiuliza ni kivipi? Tulia leo nipo kwa ajili yako. Watu ambao
wanakuzunguka ndio wana picha kamaili juu ya maisha yako.
Kwa
mfano mtu akiwa mlevi hawezi kusema mimi ni mlevi ila watu ambao
wanakuzunguka ndio ambao watasema yule jamaa ni mlevi sana. Picha
hiyohiyo ya kumuona mtu mwingine tabia yake ndiyo ambayo inatumika kujua
kipaji chako.
Hebu
waulize nyie mnanionaje, mna picha gani? Mnahisi nina kipaji Gani?
Baada ya kuwauliza hayo wao ndio watakupa picha kamili juu ya kipaji
chako na maisha yako kwa ujumla.
Soma; Jinsi Ya Kutambua Kipaji Cha Mtoto Wako Na Kukiendeleza.
3. Matatizo.
Matatizo
ni njia nzuri ya bora sana ya kugundua kipaji chako. Ulimwegu wa leo ni
ulimwengu wenye changamoto nyingi sana, hata hivyo kutokana na suala
hilo, pale matatizo yanapotokea na kuyapatia ufumbuzi sahihi hapo ndipo
utakapojua kipaji chako.
Kwa
mfano watu wengi leo hii wanapenda maisha ya kufanyiwa kila kitu.
Tuchukulie leo hii unamtegemea mtu fulani ili aweze kukutimizia lengo
lako. Halafu siku ya siku mtu huyo anakufukuza nyumbani kwake na
kukuambia nenda kajitegemee.
Baada
ya kuambiwa hivyo ndipo unakuja kugundua ni kipi kipaji chako baadala
ya kuendelea kuwa tegemezi. Hebu tuone mfano mwingine unakuta mtu
alikuwa ni mfanyakazi wa ofisini ila baada ya kustafu unajikita katika
ufugaji mwisho wa siku unagundua wewe ulikuwa una kipaji cha ufugaji
badala ya kufanya kazi za maofisini.
Hivyo wito wangu kwako ni vyema ukagundua kipaji chako mapema usisubiri changamoto fulani zitokee ndipo ugundue kipaji chako.
4. Mashindano.
Kuna
baadhi ya nchi huandaa mashindano mbalimbali kwa ajili ya kusaka
vipaji, hili jambo jema sana hata hapa kwetu nchini kuna baadhi ya
mashindano hufanyika ambayo husaidia kujua vipaji vya watu kama vile
bongo star search, fiesta, DJ compition, umiseta na mangineyo mengi.
Hivyo
kama kweli unataka kujua kipaji chako endapo yatatokea mashindano
yoyote yale jitahidi sana kwenda kushiriki kwani hii itakusaidia kwa
kiwango kikubwa kuweza kujua ni kipi kipaji chako.
Mpaka
kufikia hapo niweke nukta kwa kusema kama ukwisha kugundua hicho kipaji
chako ni vyema ukajua ni namna gani ya kugeuza hicho kipaji chako kuwa
pesa, kwani hapo ndipo palipo kuwa na changamoto kubwa.
Tuesday, September 26, 2017
KARIBU TUME YA MAENDELEO YA USHIRIKA
Popular Posts
-
📌 Asema Rais, Dkt. Samia anafanya kazi kubwa ya kuwaunganisha Watanzaia 📌 Atak...
-
Mvua kubwa za El-Nino zilizonyesha zimeleta athari maeneo mbalimbali...
-
Wafanyakazi wanawake wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Dodoma, wakiwa wamejipanga tayari kwa maandamano katika maadhimisho ya S...
-
Waziri wa Kilimo Mhe Prof Adolf Mkenda akifurahia jambo pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) ...
Powered by Blogger.
0 comments:
Post a Comment