Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akikagua upanuzi wa Hospitali ya Tumbi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akitoa maagizo kwa uongozi wa mkoa wa Pwani na watendaji wakuu wa Shirika la
Elimu Kibaha ambao Hospitali ya Tumbi ipo chini yao.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akikagua ramani ya upanuzi wa jengo la hospitali ya Tumbi Kibaha.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akimsalimiana na mgonjwa ambaye ni mlemavu wa viungo katika Hospitali ya Tumbi.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo
akipata maelezo kutoka kwa mganga mkuu wa hospitali ya Rufaa ya Tumbi iliyopo
mkoani Pwani.
...........................................................................
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo ameutaka Uongozi
wa Shirika la Elimu Kibaha na Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kukaa
pamoja na kufanya Maamuzi ya haraka ndani ya wiki moja wafikie makubaliano ya
uendelezaji wa ujenzi wa jengo jipya la upanuzi wa hospital ya Tumbi ambayo ni
hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani.
Jafo ameoneshwa kukerwa na ugoigoi wa kufanya maamuzi unaoendelea
licha ya serikali kupeleka fedha kiasi cha sh.milioni 685 katika mwaka wa fedha
2016/2017 lakini mpaka sasa wameshindwa kufanya Maamuzi.
Naibu Waziri Jafo amesema kitendo hicho kinachelewesha kuwapatia
huduma bora wananchi.
Kutokana na hali hiyo, Jafo amewaonya watendaji hao na kuagiza hadi
wiki ijayo wawe wamekamilisha mkataba wa makubaliano na ujenzi uanze mara
moja.
Upanuzi wa hospitali ya Tumbi unalenga kuimarisha miundombinu ili hospitali hiyo iweze kutoa huduma bora kwa wananchi mbalimbali wa mkoa wa pwani na mikoa mingine hapa nchini kwani kwa muda mrefu hospitali hiyo imekuwa ikipokea wagonjwa wengi kwa siku ikihusisha pia majeruhi wengi wanao pata ajali katika barabara ya Morogoro.
0 comments:
Post a Comment