Washiriki wakiwa katika mafunzo hayo
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania, Bw. Hiiti Sillo akitoa maelezo ya utangulizi kwa washiriki
Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto , Dkt.
Ulisubisya Mpoki akisisitiza jambo katika hotuba yake ya ufunguzi
Picha ya pamoja baina ya Mgeni Rasmi, Katibu
Mkuu wa Wizara ya Afya , Maendeleo ya Jamii , Jinsia , Wazee na Watoto ,
Dkt. Ulisubisya Mpoki (wa tatu kushoto, msitari wa mbele), akiwa na
waratibu, na washiriki wa mafunzo ya kutathimini kwa ulinganifu ufanisi
na usalama wa dawa katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Mamlaka ya
Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), Shirika la Afya Duniani (WHO) na
Sekeretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki wameshiriki katika uratibu
wa mafunzo hayo na kutoa misaada ya hali na mali.
…………………
Na Mwandishi Wetu, MAELEZO
Serikali imesisitiza umuhimu wa
mafunzo zaidi kwa wataalamu wa ukaguzi na udhibiti ili kuhakikisha dawa
zinazoingizwa na kutengenezwa nchini zina ubora kwa kuzingatia viwango
na vigezo vilivyowekwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk. Ulisubisya Mpoki amesema
kuwa moja ya changamoto kubwa zinazozikabili nchi nyingi barani Afrika
katika kuwapatia wananchi wake huduma bora za afya ni ukosefu wa
wataalamu wa kutosha wa ukaguzi wa dawa hivyo mafunzo ya wataalamu hao
hayana budi kupewa kipaumbele.
“Tanzania tunaagiza asilimia
themanini ya mahitaji yetu ya dawa na kutengeneza kiasi kilichobaki
hivyo suala la weledi katika ukaguzi na udhibiti wa dawa ni jambo
linalopaswa kupewa umuhimu mkubwa” Dk. Mpoki alisema.
Katibu Mkuu huyo amesema hayo leo
wakati akifungua rasmi mafunzo ya siku tisa ya ulinganishaji wa viwango
vya dawa kwa wakaguzi na wataalamu wa udhibiti wa dawa kutoka nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika kituo
Mahsusi cha Kanda cha Ukaguzi na Udhibiti wa Dawa kwa Afrika Mashariki
kilichopo Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi ya Afya, Muhimbili.
Kwa hivyo amewataka washiriki wa
mafunzo hayo kuzingatia kwa makini mafunzo hayo kwa kuwa yatawaongezea
uwezo wa kuhakikisha dawa zinazotumiwa wananchi wa nchi zao ni zenye
ubora na salama.
“Tumieni fursa ya mafunzo haya
kuhakikisha mnapata ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kufanya maamuzi
sahihi katika kuamua ubora wa dawa katika nchi zenu” Dk. Mpoki
alisisitiza.
Aliongeza kuwa kuanzishwa kwa
kituo hicho ni hatua muhimu ya kukabiliana na changamoto hiyo na kueleza
utayari na dhamira ya Serikali ya kuendelea kukiunga mkono kituo hicho
ili kiweze kutimiza majukumu yake.
Wakati huo huo, Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Hiiti Sillo amesema lengo la kituo
hicho ni kufundisha wataalamu wengi zaidi kutosheleza mahitaji ya nchi
wanachama ili kuhakikisha kazi ya ukaguzi na udhibiti wa ubora wa dawa
unaimarika katika nchi hizo.
Alifafanua kuwa katika Programu ya
Ulinganishi wa Dawa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, TFDA ndio
taasisi kiongozi wa kuratibu na kusajili dawa.
Aliongeza kuwa uamuzi wa TFDA
kupewa dhamana hiyo unatolaka na uwezo wa kitaalamu na miundombinu
iliyopo nchini katika kutekeleza jukumu hilo.
Mkurugenzi Mkuu huyo alibainisha
kuwa kituo hicho ambacho kilianzsihwa mwaka 2014 na kuanza shughuli zake
mwaka 2015 na kinaendeshwa kwa pamoja kati Jumuiya ya Afrika Mashariki,
TFDA na Shule ya Phamasi ya Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili.
0 comments:
Post a Comment