Naibu Waziri wa Afya Zanzibar Bi.
Harusi Said Suleiman akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Bohari kuu
ya Dawa Zahran Ali Hamad alipotembea kuona dawa katika bohari hiyo,
iliyopo Maruhubi Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.
…………………
Na Mwashumgi Tahir Maelezo Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar
kupitia Wizara ya Afya Zanzibar imewahakikishia wananchi kuwa Bohari
kuu ya Dawa inadawa za kutosha za kuhudumia wagonjwa wanaofika kupata
matibabu katika Mahospitali na vituo vya Afya.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu
Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman wakati alipofanya ziara katika
Bohari kuu ya Dawa na kuangalia namna ya upatikanaji wa dawa.
Amesema uwepo wa Dawa katika
Bohari kuu ya dawa nikuonesha kuwa Serikali ina imani na wananchi wake
kwa kuongeza Bajeti ya ununuzi wa dawa kwa asilimia mia moja ambapo
upungufu upo kidogo kwenye dawa za wagonjwa wa akili ambap o Wizara iko
mbioni kutatua tatizo hilo.
”‘Wananchi msininuwe dawa katika
mahospitali na vituo vya Afya zipo za kutosha kwani Serikali imefanya
jitihada kubwa ya kueneza dawa na kuzisambaza mahosptalini mote na
vituo vya afya ambapo kama kutakuwa na upungufu wa dawa Wizara tutatoa
taarifa maalum kwa wananchi wake”. Naibu Waziri huyo Alisisitiza.
Amewataka wafanyakazi wa
Mahospitalini na Vituo vya Afya kuagiza dawa kwa wakati kwani kufanya
hivyo kutasaidia kuondosha urasimu kwa wagonjwa ambao wanaokwenda kupata
huduma ya matibabu na kuwambiwa dawa hakuna ambapo kuna dawa za kutosha
katika Bohari ya dawa.
Kwa upande wa Mkurugenzi Bohari
kuu ya Dawa Zahran Ali Hamad amesema kwa mujibu wa mahitaji ya dawa
muhimu zinazotumika katika visiwa vya Unguja na Pemba dawa zipo za
kutosha kwa kuwahudumia wananchi.
Amezitaja dawa hizo ni pamoja na
za akinamama wanofika kujifungua,dawa za mpango wa uzazi, dawa ya
kisukari na pressure na maradhi mengine na kuwasisitiza wahudumu wa afya
kuagiza dawa kwa wakati.
0 comments:
Post a Comment