Na: Lilian Lundo – MAELEZO – Dodoma
Serikali kuendelea kuboresha
mazingira ya kufanyia biashara ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuvutia
wafanyabiasha wa ndani na nje ya nchi.
Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu
Hassan ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akizindua awamu ya tano
ya programu ya maboresho ya usimamizi wa fedha za Umma 2017/18 na
2021/22.
Akifafanua Mhe. Samia amesema
kwamba katika kuhakikisha kunakuwepo na usimamizi mzuri wa fedha za
umma, Serikali ya Awamu ya Tano itahakikisha kuwa wafanyabishara wote
wanatumia mfumo wa kielekroniki kulipa kodi.
Aidha amesema kuwa Serikali
itaendelea kupunguza matumizi ya fedha katika Wizara, Taasisi na Idara
zake ili fedha hizo ziweze kutumika katika kuboresha huduma za jamii.
Naye, Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Philip Mpango amesema kuwa programu ya maboresho ya usimamizi wa
fedha umeleta mafanikio makubwa ambapo umeongeza makusanyo na mapato ya
Serikali Tanzania Bara na Visiwani.
“Awamu hii ya Tano ya program ya
maboresho ya usimamizi wa fedha za Umma itaweka nguvu na kuimarisha
ofisi za wakaguzi wa mahesabu na kutambua mapungufu yaliyopo katika
ofisi hizo,” alifafanua Dkt. Mpango.
Vile vile katika awamu hii
maboresho ya kazi za wakaguzi wa ndani katika Wizara, Taasisi, Idara
pamoja mamlaka ya Serikali za mitaa nchini.
Maboresho ya programu ya usimamizu
wa fedha za Umma ulianza mwaka 1998 ikiwa ni awamu ya kwanza ambayo
ilihusisha uthibiti matumizi ya Serikali na kuchangia kukuza uchumi
endelevu.
Awamu ya pili ilifanyika mwaka 2004 – 2008 ambayo ilijikita
katika kuboresha usimamizi wa fedha za umma kwa kutumia viwango vya
kimataifa. Awamu ya tatu ilifanyika mwaka 2008 – 2012 ambayo ilihusisha
katika kuhakikisha mbinu na mifumo iliyowekwa awamu ya kwanza
inaoanishwa na kutumika ipasavyo kuleta matokeo yaliyokusudiwa na awamu
ya nne ilikuwa mwaka 2012-2017 ambayo ilenga katika nidhamu katika
usimamizi wa fedha za umma na kutoa huduma bora kwa Umma ili kuleta
maendeleo endelevu
0 comments:
Post a Comment