METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, June 26, 2019

BODI ZA HOSPITALI ZA RUFAA ZATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO

Wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali za Rufaa za Mikoa wakiwa katika kikao kazi Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya akisema jambo kwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri wa Hospitali za Rufaa za Mikoa (hawako pichani) katika Kikao kazi kilichofanyika jana Jijini Dodoma.
*************
Na.WAMJW,Dodoma Wajumbe wa bodi za ushauri za hospitali za rufaa nchini wametakiwa kutatua changamoto zilizopo kwenye hospitali zao ili wananchi wapate huduma zilizo bora.
Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu,Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Zainabu Chaula wakati akifungua kikao kazi cha uhamasishaji wa wajumbe wa bodi za ushauri za hospitali za rufaa za mikoa kinachofanyika jijini hapa Dkt.Chaula alisema wizara inawategemea na kuwathamini wajumbe hao katika kuleta mabadiliko ya uimarishaji wa huduma za afya katika hospitali za mikoa zilipo katika maeneo yao hivyo wanatakiwa kuwa wabunifu.
“Nyie ndio macho yetu kule, tumewapa wajibu hivyo tunawategemea mtushauri na kuleta mafanikio katika maeneo yenu”.Alisisitiza Dkt.Chaula
Aidha,aliwataka wabuni katika kuongeza vyanzo vya mapato ili hospitali hizo ziweze kuwahudumia wananchi ipasavyo na si kwenda hospitali za ngazi za juu.
“madaktari bingwa wanatengenezwa wananchi hawapaswi kwenda hospitali kubwa bali hospitali za rufaa”.Alisema Dkt.Chaula
Wakati huo huo Mganga Mkuu wa Serikali Pof.Mohhamad Bakari Kambi alisema wanatarajia mabadiliko makubwa katika rasiliamali watu hususan kwenye sekta ya afya kwa kuwa wabunifu.
“Tutawapima kwa utendaji na mafanikio yenu na hivyo tutapenda baadae muwe bodi tendaji ili muwe na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi na si ushauri kama ilivyo sasa”.Alisema Prof.Kambi.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Tiba Dkt.Grace Maghembe alisema wanatambua mchango wa bodi hizo kwani ndio walezi kwenye hospitali za rufaa za mikoa hivyo watasaidiana panapotokea mapungufu ili kuweza kurekebisha kwa haraka.
Dkt.Maghembe aliwataka wajumbe hao kusaidia kwa utashi katika kuimarisha na kusimamia vyanzo vyanzo vya mapato yanayokusanywa pamoja na matumizi yake na kuzifanya hospitali za rufaa za mikoa kupunguza rufaa za hospitali kubwa na kuzifanya ziwe sehemu za kwanza za rufaa na kupunguza gharama za matibabu. Kikao kazi hicho kinakutanisha wajumbe wa bodi za ushauri za hospitali za rufaa za mikoa kutoka mikoa kumi kutoka Tanzania bara.
Share:

Related Posts:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © 2025 WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com