Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli tarehe
25 Septemba, 2017 amemaliza ziara yake ya siku 6 katika Mkoa wa Arusha.
Akiwa
njiani kuelekea uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Mhe.
Rais Magufuli amesimamishwa na wananchi wa Sangsi nje kidogo ya Jiji la
Arusha na wananchi wa Pacha ya Kia Mkoani Kilimanjaro na kuwahakikishia
kuwa Serikali itaendelea kutatua kero za wananchi na kuwahudumia bila
kuwabagua kwa misingi ya itikadi za kisiasa, dini na ukabila.
Mhe.
Rais Magufuli amesema katika kutimiza azma hiyo Serikali inatekeleza
miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara ya Usa River –
Arusha inayojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 139, mradi wa maji wa
Arusha utakaogharimu Shilingi Bilioni 42, mradi wa kusambaza umeme
katika vijiji zaidi ya 200 na mingine mingi inayotekelezwa katika maeneo
hayo.
“Nina
uhakika nyinyi wakazi wa Arusha mnaona Arusha inavyobadilika, kabla ya
kujengwa barabara hii kulikuwa kunatokea ajali nyingi, na kuna watu
walikufa pale kwenye daraja, inawezekana wengine wameanza kusahau,
wanaozaliwa sasa hivi wanaweza kuona haya sio chochote lakini hii ni
ishara ya kupanda kwa uchumi wetu, uchumi unapopanda na miundominu
inakuwa mizuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Aidha,
Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero mbalimbali za wananchi wakiwemo
wafanyakazi ambao wamelalamikia kuhamishwa vituo vya kazi bila kulipwa
stahiki zao na amerejea agizo lake la kupiga marufuku mfanyakazi yeyote
kuhamishwa kituo cha kazi pasipo kulipwa stahiki zake.
Kuhusu
kero za wananchi wa pacha ya Kia waliolalamikia tatizo la uhaba wa
maji, kunyang’anywa maeneo ya biashara na waliokuwa walinzi wa uwanja wa
ndege kudai haki zao Mhe. Rais Magufuli ameziagiza mamlaka husika
kushughulikia matatizo hayo.
Mhe. Rais Magufuli amerejea Jijini Dar es Salaam.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Arusha
25 Septemba, 2017
0 comments:
Post a Comment