TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan leo amefungua mkutano wa Majaji na Mahakimu wa nchi wanachama
wa Jumuiya ya Madola akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli. Mkutano huo umefanyika katika
ukumbi wa Mikutano wa Benki Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.
Katika
uzinduzi huo, Makamu wa Rais alipongeza mafanikio makubwa yaliyofikiwa
na Chama cha Majaji na Mahakimu wa nchi wananchama wa Jumuiya ya Madola
(CMJA).
Makamu
wa Rais alisema” jitihada zenu katika kuendeleza na kuimarisha viwango
na uhuru wa mahakama na vilevile kuendeleza utawala wa sheria
vimeendelea kuimarika na kuifanya jumuiya yenu kuwa imara zaidi”.
Kwa
miaka mingi mmeendelea kuchochea na kuimarisha uhuru wa mahakama huku
mkijitahidi kuendeleza utawala wa sheria katika nchi za jumuiya ya
madola, alisema Makamu wa Rais.
Aidha,
mkutano huo uliohudhuriwa na Majaji Wakuu wa Mahakama, majaji na
mahakimu, Makamu wa Rais aliuasa mhimili wa Mahakama kuunga mkono
jitihada za serikali katika mapambano ya kuondoa umaskini na rushwa ili
kufikia maendeleo ya kweli.
“Naamini
kwamba nia ya kujenga mahakama yenye ufanisi, uwajibikaji na jumuishi
haitafikiwa kama mahakama ya Tanzania itajitenga na jitihada za serikali
za kuondoa umaskini na rushwa”, alisisitiza Makamu wa Rais.
Pia
Makamu wa Rais alisisitiza kuwa rushwa huondoa uhuru wa mahakama na
hivyo kupoteza utawala wa sheria. Aliwataka washiriki wa mkutano huo
kupambana na rushwa katika mahakama ili kuhakikisha haki na maendeleo
vinapatikana.
Mwisho
Makamu wa Rais aliwahakikishia washiriki wa mkutano huo kwamba serikali
ya Tanzania itaendelea kuheshimu na kuimarisha uhuru wa Mahakama kwa
kuhakikisha inaendelea kupambana na kuondoa vitendo vya rushwa.
Imetolewa na :-
Ofisi ya Makamu wa Rais
0 comments:
Post a Comment