Waziri
wa Utamaduni Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amepiga marufuku
mashindano ya Miss Tanzania na tuzo za muziki kutokana na ubabaishaji wa
waandaaji wa mashindano ya tasnia hizo.
Mwakyembe
amesema mashindano ya Miss Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji kwenye
utoaji wa tuzo na kumekuwa na tabia ya kuchelewa kuwapa washindi zawadi
wanazoahidiwa jambo linaloleta usumbufu.
Waziri
huyo ameongeza kuwa watakaotaka kuandaa mashindano hayo ni lazima
zawadi wanazoahidi kuwapa washindi zipekwe ofisini kwake.
”Kwa
sasa tunanakaa chini na wadau wa burudani juu ya mashindano hayo ila
tunataka tuzo ziwe na (guaranteed sustainability) muendelezo wa uhakika
na sio kufanyika kwa kubahatisha”, alisema Mwakyembe.
Kwa
mara ya mwisho mashindano ya za Miss Tanzania yalifanyika mwaka 2016
ambapo ilichukua takribani miezi 6 kwa Kamati ya shindano la Urembo la
Miss Tanzania kumpatia mshindi zawadi yake.
Kwenye
tuzo za muziki waziri Mwakyembe amesema tuzo hizo zinahitaji
marekebisho kwani zilikuwa zikitegemea watu wachache kiasi kwamba
wakinuna basi hakuna tuzo.
0 comments:
Post a Comment