Ndege
za kijeshi za Marekani zimepaa karibu na pwani ya mashariki ya Korea
Kaskazini katika kuonyesha ubabe wa kivita, idara ya ulinzi nchini
Marekani pentagon imesema.
''Hatua hiyo ni kuonyesha kuwa rais Trump ana njia tofauti za kijeshi kushinda vitisho vyovyote'' , msemaji Dana White alisema.
Marekani na Korea Kaskazini zimerushiana cheche za maneneo katika kipindi cha hivi majuzi.
Katika
Umoja wa mataifa siku ya Jumanne, bwana Trump alisema kuwa ataiangamiza
Korea Kaskazini iwapo Marekani italazimika kujitetea na washirika wake.
''Hili
ni eneo ambalo jeshi lolote halifai kupitia na ni ndege za kijeshi za
Marekani ambazo zimeweza kulifikia katika karne ya 21, licha ya tabia
mbaya ya Korea Kaskazini'', alisema Bi White.
Tangazo hili lilijiri muda mfupi kabla ya waziri wa kigeni wa Korea Kaskazini kutoa hotuba yake katika umoja wa mataifa.
Mapema
siku ya Jumamosi , tetemeko lenye ukubwa wa 3.4 katika vipimo vya
Ritcher lilisikika karibu na kituo cha kujaribia makombora cha Korea
Kaskazini na kuzua hofu kwamba taifa hilo huenda lilitekeleza jaribio
jingine la kombora lake.
Lakini wataalam wamesema kuwa lilikuwa tetemeko la ardhi.
0 comments:
Post a Comment