METDO Tanzania

METDO Tanzania

Friday, May 25, 2018

HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO YAZINDUA BODI YA AFYA

Na Bornwell Kapinga, Dar es salaaam

Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo leo imeweka historia ya kuzindua Bodi yake ya Afya katika ukumbi wa Mikutano ulioko makao makuu ya Manispaa hiyo Kibamba CCM Jijini Dar es Salaam.

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Mkuu wa wilaya ya Ubungo Mheshimiwa Kisare Makori

Akitoa taarifa ya afya kabla ya uzinduzi huo kaimu mganga mkuu wa Manispaa  Dr Mariam Malliwa alifafanua majukumu ya idara ya afya katika Manispaa ya Ubungo akibainisha mafanikio na mpango mkakati wa siku za usoni ikiwemo pamoja na kujenga zahanati ,vituo vya afya na Hospitali ya Wilaya ili kuleta huduma za afya karibu na wananchi.

Baada ya taarifa iliyotolewa na Mganga mkuu wa Manispaa, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John L.Kayombo alimkaribisha mgeni rasmi kwa ajili ya kutoa hotuba na kufanya uzinduzi wa Bodi hiyo.

Mgeni rasmi Mhe Kisare Makori akitoa hotuba kwa wajumbe hao wapya wa Bodi na amewapongeza kwa kupata nafasi hiyo ya kuwa wajumbe wa Bodi ya Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo.

Aliwaambia Bodi hiyo ambayo ataizundua ipo kwa mujibu wa katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ni vyema ikafanya kazi kwa kuzingatia uwazi, uwajibikaji na weledi kwa lengo la kutoa huduma bora za afya kwa jamii.

Amehimiza nafasi hiyo waitendee haki kwa kuwa sekta ya afya ni muhimu kwa mstakabali wa maisha ya jamii hususani jamii ya Ubungo na kila mmoja wao anapaswa kuwa na mchango chanya.

"Naiomba Bodi hii kila inachokifanya ifanye tafiti ili kuwa na uwezo mkubwa  wa kufanya kazi kwa ustadi pia kuwa na mfumo mzuri wa kuwasiliana au mawasiliano katika kila jambo linalohusu Bodi hiyo" alisema *Makori*

Baada ya hotuba hiyo Mkuu wa wilaya ya ubungo Mhe *Kisare Makori* alitamka rasmi kuwa Bodi hiyo mpya ya Halmashauri imezinduliwa.

Aidha baada ya kuzinduliwa Bodi hiyo ya afya ukafanyika uchaguzi wa Mwenyekiti wa Bodi ambapo Ndg *Israel Sosthenes* akaibuka kidedea na kushinda nafasi ya Uwenyekiti wa Bodi mpya ya afya Halmashauri ya Ubungo

Mwenyekiti huyo alipata nafasi ya kushukuru na kuhaidi atatoa ushirikiano kwa wajumbe wote wa Bodi ili kuweza kuboresha utoaji wa huduma ya afya iliyo bora katika jamii ya Ubungo.

Naye mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg *John L.Kayombo* ambaye pia ni mjumbe wa Bodi hiyo amesema sekta ya afya inachangamoto nyingi ninawaomba wajumbe wote tushirikiane bega kwa bega katika kuhakisha huduma za afya katika manispaa ya Ubungo zinaboreshwa.

MWISHO

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com