Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack
akizindua kampeni ya upandaji miti ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ leo
Septemba 23,2017-Picha na Kadama Malunde – Malunde1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro ameanzisha kampeni ya upandaji miti yenye kauli mbiu
ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ ili kuboresha mazingira na kupambana na
mabadiliko ya tabia nchi yanayosababisha jangwa katika wilaya hiyo.
Kampeni hiyo imezinduliwa leo Jumamosi
Septemba 23,2017 katika manispaa ya Shinyanga na Mkuu wa mkoa wa
Shinyanga,Zainab Telack kwa lengo la kuboresha mazingira ya mji wa
Shinyanga,maeneo ya taasisi,maeneo ya wazi,maeneo yanayozunguka
kaya,kandokando ya barabara na sehemu zingine ambazo hazina miti.
Akizindua kampeni hiyo,Telack alisema
kutokana na mvua haba katika mkoa wa Shinyanga, kumekuwepo na mabadiliko
ya tabia nchi hali inayosababisha kuwepo na hali ya jangwa.
Telack aliwataka wananchi na wadau wote kuhakikisha wanatunza miti hiyo na kuzuia mifugo kuzurura ovyo mitaani.
“Tutakuwa wakali,kuanzia sasa ni
marufuku kwa mifugo kuzurura mitaani,ikikamatwa kwa kila mfugo faini ni
kati ya shilingi 50,000/= na 100,000/=,iwe ng’ombe,mbuzi,kondoo au
punda, tukikuta mti umekauka faini ni shilingi 50,000/=”,alieleza mkuu
huyo wa mkoa.
Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,
Josephine Matiro alisema uzinduzi wa kampeni hiyo umeanza na barabara 25
za mji wa Shinyanga ambapo jumla ya miti 3000 imepandwa na ofisi zote
kata 17 za manispaa ya Shinyanga zitaendelea kutekeleza zoezi hilo.
Alibainisha kuwa ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,sasa
wilaya hiyo imekuja na teknolojia rahisi ya kumwagilia miti kwa njia ya
matone,teknolojia ambayo inatumia maji kidogo lakini inaweza kumwagilia
miti mingi na kwa muda wote.
“Tumekuwa tukipanda miti kila mwaka lakini miti hii ilikumbwa na changamoto nyingi wakati wa usimamizi na kusababisha miti mingi kufa,kwa sasa tumekuja na mpango huu mpya wa kupanda miti itayosimamiwa na wananchi na wadau wote”,alieleza Matiro.
Alisema kauli mbiu hiyo ya Upandaji
miti ya ‘Shinyanga Mpya,Mti Kwanza’ ina maana ya kuwaasa watu wote wa
Shinyanga kuachana na tabia ya kuharibu miti na hivyo wahifadhi miti.
“Tutatekeleza kampeni hii katika
halmashauri zote,kila halmashauri itaanzisha kitalu na kuzalisha miche
isiyopungua 25,000,kila kata ipande miti isiyopungua 1000 na iwe na
kitalu cha kudumu,ofisi za mitaa na vijiji miti 100,vitongoji miti
50,kila mwananchi miti isiyopungua mitatu na taasisi zote zipande
miti”,alifafanua Matiro.
Aliongeza kuwa ili kufanikisha kampeni
hiyo,taasisi mbalimbali zitachangia mbegu,miche na kupanda miti ili
kufikia lengo la kupanda miti isiyopungua milioni 1,500,000 kwa mwaka.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack
akizungumza wakati wa kuzindua kampeni ya upandaji miti ‘Shinyanga
Mpya,Mti Kwanza’ leo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.Kushoto
ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga,Geofrey Mwangulumbi.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiteta jambo na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro wakati wa uzinduzi huo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo ya upandaji miti
ambapo alisema miongoni mwa malengo yake ni kuhifadhi ardhi na
kuiongezea thamani,kuzuia mmomonyoko wa adhi na kuboresha mazingira
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo.Alieleza kuwa kila
kiongozi akialikwa kwenye tukio lolote,kabla ya shughuli ni vyema
kwanza apande mti.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro akisisitiza kuwa kampeni hiyo inalenga kujinasua na athari za
mabadiliko ya tabia nchi.
Wananchi wakiwa wameshikilia vijiti vinavyotumika katika zoezi la upandaji miti.
Uzinduzi unaendelea
Mdau wa Mazingira Ezra Manjerenga akieleza namna ya kupanda miti hiyo.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akipanda mti nje ya ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Shinyanga.
Wananchi wakishuhudia mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akipanda mti.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akichomeka vijiti kwenye mti aliopanda.
Meneja wa Benki ya CRDB,Said Pamui
akipanda mti nje ya ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga wakati wa
uzinduzi wa kampeni ya upandaji miti ‘Shinyanga mpya,mti kwanza’.
Wafanyakazi wa benki ya CRDB na wananchi wakishuhudia Meneja wa Benki ya CRDB,Said Pamui akipanda mti.
Meneja wa Benki ya CRDB,Said Pamui akishindilia udongo kwenye mti alioupanda.
Wananchi wakitoka katika ofisi ya mkuu
wa wilaya ya Shinyanga wakielekea kwenye barabara mbalimbali mjini
Shinyanga kwa ajili ya kupanda miti.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akiweka udongo kwenye mti alioupanda nje ya ofisi ya CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack akiwa katika ofisi ya CCM wilaya ya Shinyanga mjini.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine
Matiro akichimba shimo kwa ajili ya kupanda mti katika barabara ya
Hospitali ya mkoa wa Shinyanga.
Mwananchi akifurahia baada ya kumaliza kupanda mti katika Barabara ya Shinyanga – Mwanza.
0 comments:
Post a Comment