Na Augustino Chiwinga
Watanzania wapuuzeni wapinzani wanaodai kwamba Serikali ya Chama Cha Mapinduzi haijafanya maendeleo yoyote , wapinzani hao wanawapotosha na kuwadanganya wananchi hali ya kuwa wananchi wenyewe ni mashahidi wa jinsi nchi inavyopiga hatua ya kimaendeleo siku baada ya siku.
Nashangazwa na watu hao wanaosema hakuna maendeleo yoyote yaliyopatikana wakati wanatembea katika barabara za nzuri za lami zilizojengwa na CCM, wanakunywa maji yaliyoletwa na CCM wanatumia nishati ya umeme ulioletwa na CCM na hata wakiumwa wanapata matibabu kwenye hospital zilizojengwa na CCM.
Siku hizi vijiji vingi vina huduma ya Maji na Umeme wa REA ,Hospitali na Vituo vya Afya na Zahanati, Mashule kila kona, Wanafunzi wanasoma bure , Mikopo ya Elimu ya
Juu inatolewa, Viwanda vinajengwa, Vijana na Wanawake wanakopeshwa fedha na Serikali ya CCM, Wazee juu ya miaka 60 wanatibiwa bure katika Hospitali za Serikali, Wakulima wanapewa ruzuku za pembejeo za kilimo, kwa mara ya kwanza CCM inajenga reli ya kisasa ya kimataifa itakayotumiwa ns treni ya umeme, Mtandao wa barabara za lami umepanuka hivyo sio jambo la kiungwana kwa mtu kudai kwamba hakuna maendeleo yoyote yaliyofanywa na Chama Cha Mapinduzi
Ni ukweli kwamba maendeleo ya mwanadamu hayana mwisho. Hata Tanzania ikifanikiwa kwa kiwango kikubwa kiasi gani, bado hayo hayatakua maendeleo ya mwisho, yaani maendeleo ya juu kabisa.
Kila hatua katika maendeleo ya mwanadamu, huvutia hatua nyingine tena na huendelea hivyo hadi mwisho wa maisha yetu ambapo hujitokeza vizazi vingine na kuendeleza pale tulipoishia.
Kutokana na msingi huo, ndio maana hata nchi zilizoendelea sana duniani, hazijawahi kufika mahali zikaridhika na maendeleo yake bali kila Siku Serikali zao zinajitahidi kupasua vichwa kuona ni vipi wafanye ili waweze kuendelea zaidi.
Ni jambo la wazi kuwa mambo mengi mazuri ambayo yana manufaa makubwa kwa taifa letu na yamefanywa na Chama Cha Mapinduzi hivyo kinafaa kuungwa mkono na wananchi wote.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) bado hakijabadilisha asili ya kuanzishwa kwake ambayo ni kuwa chama cha kijamaa kinachojishughulisha na kutatua shida za watu na hivyo kitaendelea kuweka juhudi ili kutatua kero na kuleta maendeleo kwa wananchi kwa wakati husika na kwa kulingana na mahitaji ya kipindi hiko.
0 comments:
Post a Comment