Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam,Paul Makonda jana amefunga rasmi zoezi
la Siku tano la Upimaji wa Afya Bure kwa Wananchi wa Dar es salaam,
ambapo amewasihi Wananchi kujiwekea utaratibu wa kupima Afya zao mara
kwamara.
Hadi kufikia majira ya Mchana zaidi ya Wananchi 11,000 walikuwa
tayari wamepimwa afya zao, Makonda amesema lengo ni kuhakikisha Wananchi
wote zaidi ya 20,000 waliohudhuria wanapimwa na watakaobainika kuwa na
matatizo ya kiafya Wanapatiwa Matibabu.
Makonda amewashukuru Madaktari,Wauguzi,Askari Polisi, Vyombo vya
Habari,Watu wa Usafi na Wadau wote waliojitoa kumuunga mkono hadi
kufanikisha zoezi hilo.
Amesema kuwa Zoezi hilo la Siku tano limefanikiwa kwa 100% huku
likigharimu kiasi cha zaidi ya Shilling Billioni Moja ikihusisha
Vipimo,Matibabu,Vyakula, Vinywaji ambapo gharama zote hizo zimegharamiwa
na Wadau wa Maendeleo waliojitolea kumuunga mkono RC Makonda
Aidha RC Makonda amewapongeza Wananchi wote waliojitokeza na
kuchangia Damu kwakuwa kiasi cha Damu walizochangia zitakwenda kuokoa
maisha ya Wagonjwa.
Upimaji wa Afya ulihusisha Magonjwa yote ikiwemo Saratani, Kisukari,
Presha, Macho, Homa ya Ini na Ugonjwa wa Moyo ikihusisha Madaktari
bingwa na Wauguzi zaidi ya 300 kutoka Hospital zaUmma, Jeshi na za Watu
Binafsi.
0 comments:
Post a Comment