METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, January 18, 2021

Vijana Wanapaswa Kutumia Vikundi Ili Kujiletea Maendeleo

 Na Saleh Ramadhani.
Kikundi cha mosesco kilichopo jijini Dar es salaam kimebainisha kuwa endapo vijana wataunda vikundi mbalimbali vya maendeleo yao wanauwezo wa kuaga umasikini kwa asilimia 90 ambapo watavitumia vikundi hivyo kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla.

Hayo yamebainisha leo na Mwenyekiti wa kikundi cha Mosesco kilichopo jijini Dar es salam Bw. Tamimu Gau amesema kuwa vijana wanapaswa kuvitumia vizuri vikundi walivyonavyo ili  kujiletea maendeleo wao kwa wao.

Bw.Tamimu Gau amedai kuwa asilimia kubwa ya vijana wameridhika na maisha waliyonayo na kushinda kutwa kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo haliendani na kasi ya Maendeleo.

"inasikitisha sana binafsi nikiwaona vijana wanaanzisha magrupu kwenye mitandao ya kijamii halafu mwishoe wanadai maisha magumu,wakati kipindi hiki mvua zinanyesha wajikite hata kwenye kilimo lakini wao muda mwingi wanautumia kuchati na kudai serikali imebana hela,inasikitisha sana" Amesema tamimu

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa kuanzishwa kwa kikundi hicho ni Kuwa kikundi bora cha vijana Tanzania cha kuinuana kiuchumi na kusaidiana katika shida mbalimbali.

"Tunakusanya michango kutoka kwa wanachama, kubuni na kuanzisha miradi mbalimbali ya kiuchumi kwa lengo la kukuza uchumi wa kikundi, faida za biashara ambazo zitapatikana ndani ya mwaka husika, mwisho wa mwaka zitagawanywa kwa kila mwanachama kulingana na kiasi alichonacho kwenye akiba yake kuu pamoja na namna mwanachama anavyolipa ada kwa wakati" amesema.

Hata hivyo Bw Tamimu amedai kuwa lengo la kikundi ni kusaidiana kwa hali na mali, katika shida na raha na kufanya matendo ya huruma kwa wanajamii wenye mahitaji mbalimbali kama vile Kuwatembelea watoto yatima katika vituo vyao,Kuwafariji wagonjwa mahospitalini, Kusaidia /kushiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii na Kushirikiana na vikundi mbalimbali nchini.

" Tulitoa msaada kwa hospital ya wilaya ya kondoa mkoani Dodoma,Magodoro sita na mito sita yenye Thamani ya Million 1.2 kwajili ya wagonjwa wanaolazwa katika hospital hiyo, pia tulitembelea kituo cha watoto yatima kilichopo bicha wilaya ya kondoa,haya yote tunayafanya kwa huruma zetu kama wanakikundi na kuiunga mkono serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania" Amesema.

Kwa upande wao wanakikundi akiwemo Yusuph Kidunda na Hafsa Matata wamesema kuwa kikundi cha Mosesco kinawapa faraja sana hususani pale panapotokea tatizo lolote ima liwe la msiba basi kikundi kinasaidia kwa uharaka na kufarijiana jambo ambalo linatia moyo kwa kiasi kikubwa sana.

"Tunajivunia sana tena sana kwa kikundi hiki cha Mosesco,kwakweli kimekuwa msaada mkubwa sana kwetu,pia tumesaidia vituo vya watoto yatima kwa lengo la kuwafariji na kuwatia moyo,lakini pia tunautaratibu wa kuwatembelea wagonjwa wetu hospitalin na kushiriki shughuli za serikali ikiwemo makongamano na madhimisho kama vile maadhimisho ya ukimwi duniani na Maadhimisho ya siku ya mazingira duniani nk." wamesema.

kikundi cha vijana  wa mosesco kilianzishwa mwaka  2015 kikiwa na wanachama 19 ambapo kwasasa kinawanachama 34 kwa lengo la kusaidiana kwa hali na mali katika shida na raha na kufanya matendo ya huruma kwa jamii yenye mahitaji mbalimbali.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com