METDO Tanzania

METDO Tanzania

Monday, September 11, 2017

DC MTATURU AFANYA MAZUNGUMZO NA UONGOZI WA MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA

Kikao cha mawasilisho ya namna ya kuimarisha ufaulu wa wanafunzi katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Mtaturu, Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi Alhaji Salum Mohamed Chima pamoja na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi Mwl Athuman Salum wakati kwa upande wa TEA waliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa TEA Ndg Mussa Mzenga, Meneja Uhusiano wa mawasiliano Ndg Slivia T. Lupembe na Kaimu Meneja msaidizi wa elimu (Manager Education Support) Ndg Anne Mulimuka
Picha ya pamoja baina ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Mtaturu, Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi Alhaji Salum Mohamed Chima pamoja, Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ikungi Mwl Athuman Salum wakati, Kaimu Mkurugenzi wa TEA Ndg Mussa Mzenga, Meneja Uhusiano wa mawasiliano Ndg Slivia T. Lupembe na Kaimu Meneja msaidizi wa elimu (Manager Education Support) Ndg Anne Mulimuka

Na Mathias Canal, Dar es salaam

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu leo Septemba 11, 2017 amekutana na kufanya mazungumzo na Uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority-TEA) ofisini kwao Mtaa wa Mikocheni Jijini Dar es salaam.

Katika mazungumzo hayo Mhe Mtaturu aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi Alhaji Salum Mohamed Chima pamoja na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi Mwl Athuman Salum wakati kwa upande wa TEA waliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa TEA Ndg Mussa Mzenga, Meneja Uhusiano wa mawasiliano Ndg Slivia T. Lupembe na Kaimu Meneja msaidizi wa elimu (Manager Education Support) Ndg Anne Mulimuka.

Katika mazungumzo hayo Mhe Mtaturu aliwasilisha mpango mkakati wa kuboresha elimu katika Wilaya ya Ikungi ambayo ina namna imara ya kuinunua kiwango cha ufaulu katika Wilaya hiyo sambamba na kuimarisha mazingira ya kujifunzia na makazi kwa walimu.

Aidha, Uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority-TEA) umesaidia mashine za kuchapishia mitihani (Thermofom Machine) kwa ajili ya wasioona na vifaa vingine vyenye thamani ya Shilingi milioni 45 ambazo zipo kwenye hatua za manunuzi kwa ajili ya kuisaidia shule ya msingi Ikungi mchanganyiko. Ombi lililowasilishwa na Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi Mwezi Februari mwaka huu.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa TEA Ndg Mussa Mzenga alisema kuwa Kazi yao kubwa huwa ni kusaidia uboreshaji wa miundombinu kwa wadau wa elimu wanaoonyesha nia ya kusaidia uboreshaji wa sekta ya elimu.

Mzenga ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwa kubuni jambo hilo huku akiahidi kuunga mkono juhudi hizo kwa manufaa ya wananchi wa Wilaya hiyo.

Mhe Mtaturu alisema kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu Wilayani Ikungi ikiwa ni pamoja na Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi jambo ambalo lilipelekea kuwa na Wazo la kuanzisha Mfuko wa Elimu.

Agosti 19, 2017 Mhe Mtaturu alianzisha mashindano ya mpira wa miguu Wilayani Ikungi yanayojulikana kama IKUNGI ELIMU CUP 2017 yenye dhamira ya kuchochea hamasa kwa wananchi ya kuchangia uboreshaji wa sekta ya elimu sambamba na kuibua vipaji kwa vijana kwani itakuwa fursa ya ajira kupitia michezo.

MWISHO. 
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com