Kikao cha mawasilisho ya namna ya kuimarisha ufaulu wa wanafunzi katika Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida kikiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Mtaturu, Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi
Alhaji Salum Mohamed Chima pamoja na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi
Mwl Athuman Salum wakati kwa upande wa TEA waliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa
TEA Ndg Mussa Mzenga, Meneja Uhusiano wa mawasiliano Ndg Slivia T. Lupembe na
Kaimu Meneja msaidizi wa elimu (Manager Education
Support) Ndg Anne Mulimuka.
Picha ya pamoja baina ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Mtaturu, Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi
Alhaji Salum Mohamed Chima pamoja, Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Ikungi
Mwl Athuman Salum wakati, Kaimu Mkurugenzi wa
TEA Ndg Mussa Mzenga, Meneja Uhusiano wa mawasiliano Ndg Slivia T. Lupembe na
Kaimu Meneja msaidizi wa elimu (Manager Education
Support) Ndg Anne Mulimuka.
Na Mathias Canal, Dar
es salaam
Mkuu wa Wilaya ya
Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu leo Septemba 11, 2017 amekutana na kufanya
mazungumzo na Uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education
Authority-TEA) ofisini kwao Mtaa wa Mikocheni Jijini Dar es salaam.
Katika mazungumzo hayo
Mhe Mtaturu aliambatana na Makamu Mwenyekiti wa Mfuko wa Elimu Wilaya ya Ikungi
Alhaji Salum Mohamed Chima pamoja na Afisa Elimu Sekondari wa Wilaya ya Ikungi
Mwl Athuman Salum wakati kwa upande wa TEA waliongozwa na Kaimu Mkurugenzi wa
TEA Ndg Mussa Mzenga, Meneja Uhusiano wa mawasiliano Ndg Slivia T. Lupembe na
Kaimu Meneja msaidizi wa elimu (Manager Education
Support) Ndg Anne Mulimuka.
Katika mazungumzo hayo Mhe
Mtaturu aliwasilisha mpango mkakati wa kuboresha
elimu katika Wilaya ya Ikungi ambayo ina namna imara ya kuinunua kiwango cha
ufaulu katika Wilaya hiyo sambamba na kuimarisha mazingira ya kujifunzia na makazi
kwa walimu.
Aidha, Uongozi wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (Tanzania Education Authority-TEA) umesaidia mashine za kuchapishia mitihani (Thermofom Machine) kwa ajili ya
wasioona na vifaa vingine vyenye thamani ya Shilingi milioni 45 ambazo zipo
kwenye hatua za manunuzi kwa ajili ya kuisaidia shule ya msingi Ikungi
mchanganyiko. Ombi lililowasilishwa na Mkuu huyo wa Wilaya ya Ikungi Mwezi Februari mwaka huu.
Kwa upande wake Kaimu
Mkurugenzi wa TEA Ndg Mussa Mzenga alisema kuwa Kazi
yao kubwa huwa ni kusaidia uboreshaji wa miundombinu kwa wadau wa elimu
wanaoonyesha nia ya kusaidia uboreshaji wa sekta ya elimu.
Mzenga
ameipongeza Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ikungi kwa kubuni jambo hilo huku
akiahidi kuunga mkono juhudi hizo kwa manufaa ya wananchi wa Wilaya hiyo.
Mhe Mtaturu alisema
kuwa zipo changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu Wilayani Ikungi
ikiwa ni pamoja na Upungufu wa nyumba za walimu, Vyumba vya madarasa, Ofisi za
walimu, Maabara, Thamani mbalimbali, Matundu ya vyoo vya walimu na wanafunzi
jambo ambalo lilipelekea kuwa na Wazo la kuanzisha Mfuko wa Elimu.
Agosti 19, 2017 Mhe
Mtaturu alianzisha mashindano ya mpira wa miguu Wilayani Ikungi yanayojulikana
kama IKUNGI ELIMU CUP 2017 yenye
dhamira ya kuchochea hamasa kwa
wananchi ya kuchangia uboreshaji wa sekta ya elimu sambamba na kuibua vipaji
kwa vijana kwani itakuwa fursa ya ajira kupitia michezo.
MWISHO.
No comments:
Post a Comment