Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza na
waendesha bodaboda na baiskeli ‘daladala’ leo mjini Shinyanga-Picha na
Kadama Malunde-Malunde1 blog
****
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba ameagiza waendesha
bodaboda wote nchini kuhakikisha kuwa wanakuwa na kofia ngumu ‘Helmet’
ndani ya mwezi mmoja baada ya hapo hatua kali zitachukuliwa.
Mheshimiwa
Nchemba ametoa agizo hilo leo Jumamosi Agosti 26,2017 mjini Shinyanga
wakati akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli ‘daladala’ zaidi ya
300 wanaofanya shughuli zao katika manispaa ya Shinyanga.
Alisema
kosa la kutovaa kofia ngumu litawahusu wamiliki wa bodaboda,waendesha
bodaboda pamoja na abiria ambao kwa pamoja watawajibika kila mmoja kwa
nafasi yake.
“Hili
litafsiriwe vizuri kila eneo katika nchi yetu,kwanza kabisa kama
mmiliki hajaweka kofia mbili,bodaboda ikikutwa haina kofia mbili,tatizo
lile linaenda kwa mmiliki,pili kama mwendesha bodaboda amepewa kofia
mbili halafu akaamua kuziacha huyo ana kosa”,alieleza.
“Tatu,
kama mwendesha bodaboda ana kofia zote mbili lakini mbebwaji/abiria
hataki kuvaa kofia,mwacheni mwenye pikipiki aende na pikipiki yake,huyo
mbebwaji atakuwa na kosa la kuhatarisha maisha yake ili kila mmoja
atimize wajibu wake”,aliongeza Nchemba.
Mheshimiwa
Nchemba pia alisisitiza umuhimu wa abiria wanaopanda katika bodaboda
kukaa mkao wa kiume ili kuepusha ajali za barabarani.
Katika
hatua nyingine Waziri huyo amepiga marufuku ukamataji wa bodaboda
unaofanywa na askari polisi kwa kufukuzana na waendesha bodaboda kwani
inachangia kutokea kwa ajali.
“Tumeelekeza
ukamataji wa kistaarabu,ukamataji huu wa kistaarabu ufanyike kwa nyinyi
mtimize wajibu ili kuwe na tofauti ya aliyekosa na ambaye hajakosa,na
sisi askari lazima tutofautishe aliyekosa na ambaye hajakosa ili tuwe
marafiki na hawa watu”,alisema Nchemba.
“Tunafanya
haya kwa ajili ya maisha yenu,hatuna upendo zaidi ya kuokoa maisha
yenu,hatutaki watu wapoteze maisha kwa sababu ya uzembe wa waendesha
bodaboda ama abiria”,aliongeza Nchemba.
Naye
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule alisema kikao hicho
cha Waziri wa Mambo ya Ndani ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu ya
jeshi la polisi katika zoezi la utoaji elimu kuhusu masuala ya usalama
barabarani.
“Hivi
karibuni katika mkutano wa mkuu wa mkoa wa Shinyanga,uliolenga
kusikiliza kero za wananchi,kuna mambo yaliibuliwa ikiwemo la waendesha
bodaboda kutofahamu matumizi mazuri ya Mzunguko wa barabara ‘Round
About’ hivyo tunatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya Round about”,alieleza Kamanda Haule.
Kwa
upande wake Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack,alisema
ajali za barabarani zimepungua kutokana na waendesha bodaboda kuendelea
kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Mbunge
wa jimbo la Shinyanga Mjini,Mheshimiwa Stephen Masele (CCM) aliwataka
waendesha bodaboda kufuata sheria za usalama barabarani na askari polisi
waache kutumia nguvu kubwa kukabiliana na waendesha bodaboda.
MSIKILIZE HAPA WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AKITOA MAAGIZO LEO SHINYANGA
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza na
waendesha bodaboda na baiskeli ‘daladala’ leo mjini Shinyanga.Kulia ni
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule.Kushoto ni Mkuu wa
mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akiwasisitiza waendesha bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza.
Waendesha bodaboda na baiskeli mjini Shinyanga wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akizungumza na waendesha bodaboda na baiskeli.
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Mheshimiwa Zainab Telack akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akizungumza wakati wa kikao hicho.
Kamanda
wa polisi mkoa wa Shinyanga,ACP Simon Haule akieleza namna jeshi la
polisi linafanya ili kuhakikisha ajali za barabarani zinapungua mkoani
Shinyanga.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoa wa Shinyanga,Anthony Masanzu akisisitiza jambo wakati kikao hicho.
Mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini,Mheshimiwa Stephen Masele (CCM) akizungumza katika kikao hicho.
Kikao kinaendelea.
Mmoja wa waendesha akiuliza swali kwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mheshimiwa Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufunga kikao hicho.
Mkazi wa Shinyanga Mjini akieleza shida yake kwa Waziri wa Mambo ya Ndani,Mheshimiwa Mwigulu Nchemba baada ya kikao kufungwa.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog
0 comments:
Post a Comment