Kocha Mkuu wa timu ya Mpira wa
Miguu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, Salum Shabani Mayanga ametangaza kikosi
kipya kitakachocheza na Botswana katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa
chini ya utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa
Miguu (FIFA).
Wiki ya FIFA kwa mechi za
kimataifa inatarajiwa kuanza Jumatatu Agosti 28 hadi Septemba 2, mwaka
huu ambako Tanzania imekubaliana kucheza Botswana kwenye Uwanja wa Uhuru
jijini Dar es Salaam Jumamosi ya Septemba 2, 2017.
Katika kikosi hicho cha wachezaji
21, Kocha Mayanga amemwita upya Mlinzi wa Young Africans, Kelvin
Yondani huku nyota kutoka nje ya mipaka ya Tanzania wakiwa ni saba
akiwamo nahodha wa kikosi hicho, Mbwana Ally Samatta.
Kikosi hicho kinachotarajia
kuingia kambini kesho Jumapili kuanzia saa 2.00 usiku ni makipa Aishi
Manula (Simba SC), Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young
Africans).
Walinzi ni Gadiel Michael (Young
Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika
Kusini), Kelvin Yondani (Young Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na
Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao – Nahodha
Msaidizi (Azam FC), Hamis Abdallah (Sony Sugar/Kenya), Mzamiru Yassin
(Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Saimon Msuva (Difaa El
Jadidah/Morocco), Shiza Kichuya (Simba SC), Farid Mussa (CD
Tenerif/Hispania) na Orgenes Mollel (FC Famalicao/Ureno).
Washambuliaji ni Raphael Daud
(Young Africans), Kelvin Sabato (Azam FC), Mbwana Samatta (KRC
Genk/Ubelgiji) na Elias Maguli (Dhofar FC/Oman).
Benchi la Ufundi la Mayanga
linaundwa na yeye mwenyewe ambaye ni Kocha Mkuu, Fulgence Novatus (Kocha
Msaidizi), Patrick Mwangata (Kocha wa Makipa), Danny Msangi (Meneja),
Dkt. Richard Yomba (Daktari wa timu), Dkt. Gilbert Kigadye (Daktari wa
Viungo) na Ally Ruvu (Mtunza Vifaa).
0 comments:
Post a Comment