"Nasema tena hakuna mgombea atakayepitishwa na vikao vyetu ikiwa sifa zake zina kasoro, mapungufu au za kuokoteza okoteza , tutampekua kila mgombea na tukimuona hatokani na CCM tutamtosa bila ya kuutazama uso wake" - Shaka
"UVCCM imekusudia kurudisha nidhamu ya Chama hasa katika suala zima la kugombea nafasi za uongozi na haki ya kuchagua au kuchaguliwa" - Shaka
"Ni marufuku na hatakiwi kabisa muomba nafasi yoyote ile Mara baada kuchukua au kurejesha fomu kuandika bango au kipepeprushi na kuvigawa, kuvieneza au kuwatuma wapambe wake wakati taratibu nyengine za vikao bado hazijakamilika" - Shaka
"Ni marufuku na haitaruhusiwa kabisa muda ukifika kwa mgombea yeyote kufanya kampeni za kihuni kwa kutumia lugha chafu, siasa za maji taka, matusi, dharau kinyume na ubinadamu pia kushiriki kejeli dhidi ya wenzake" - Shaka
"Waomba nafasi hawaruhusiwa kutembea toka Wilaya au Mkoa mmoja hadi mwingine, kukusanya wajumbe, kujinadi au kuelezea dhamira yake ya kuchukua fomu kabla ya siku ya uchaguzi kwani kuyaachia hayo na mengine yafanyike huko ni kuipalilia rushwa istawi ndani ya chaguzi zetu" - Shaka
"Uchaguzi ni kipimo cha ukomavu wa demokrasia ya kweli bila kufanyika mizengwe na hila ndani ya jumuiya kwa lengo la kusimamia shabaha na misingi sahihi itokanayo na miongozo, maelekezo na kuheshimu utaratibu unaohimizwa na Chama Cha Mapinduzi na kutii maelekezo yanayotolewa mara kwa mara na Mwenyekiti wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli" - Shaka
0 comments:
Post a Comment