Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akiwa ameshikilia vifaa vya
kuchomelea vyuma kuashiria kuanza kuweka msingi wa kivuko ‘’Keel
Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa
ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma kati ya Kigongo na Busisi
Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo
Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu akichomelea vyuma kuashiria kuweka
msingi wa kivuko ‘’Keel Laying’’ katika eneo la Pasiansi ikiwa ni
kumbukumbu ya kuanza rasmi kwa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa
huduma kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa kivuko hicho
unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya
shilingi Bilioni 8.9.
Meneja wa Miradi wa Kampuni ya
Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major
Songoro (kushoto) akitoa maelezo kwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kulia) kuhusu kuanza kwa mradi wa
ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa
kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu
jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
Meneja wa Miradi wa Kampuni ya
Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major
Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) michoro itakayotumika katika
Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Ujenzi wa
kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu
jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
Meneja wa miradi wa Kampuni ya
Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Major
Songoro (kulia) akimuonyesha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu (katikati) michoro itakayotumika katika
Ujenzi wa kivuko kipya cha Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Kushoto ni
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Songoro Bwana Salehe Songoro. Ujenzi
wa kivuko hicho unatarajiwa kukamilika ifikapo Januari 2018 na
utagharimu jumla ya shilingi Bilioni 8.9.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya
Kizalendo ya MS. Songoro Marine Transport Limited ya Jijini Mwanza Bwana
Salehe Songoro (wa pili kulia aliyenyoosha mkono) akimuonyesha
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu
(wa tatu kushoto) mojawapo ya malighafi itakayotumika katika ujenzi wa
kivuko kipya cha Kigongo na Busisi. Ujenzi wa kivuko hicho unatarajiwa
kukamilika ifikapo Januari 2018 na utagharimu jumla ya shilingi Bilioni
8.9. (PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO (TEMESA MWANZA)
Na Alfred Mgweno (TEMESA MWANZA)
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme (TEMESA) Dkt. Mussa Mgwatu, ameshiriki katika zoezi la kuweka
msingi wa ujenzi wa kivuko kipya kitakachotoa huduma ya usafiri katika
Ziwa Victoria kati ya Kigongo na Busisi Mkoani Mwanza. Zoezi hilo
linaloashiria kuanza rasmi kwa ujenzi huo limefanyika Pasiansi katika
eneo linalotumika kwa ajili ya ujenzi wa meli, vivuko na boti
linalomilikiwa na Kampuni ya Songoro Marine Transport Limited ya Mwanza
iliyoshinda zabuni ya kujenga kivuko hicho kwa gharama ya Shilingi
Bilioni 8.9 za kitanzania.
Tukio hili la kihistoria lilihudhuriwa pia na
Mkurugenzi wa Ukodishaji Mitambo na Huduma za Vivuko kutoka TEMESA
Mhandisi Japhet Y. Maselle, Mhandisi Amos Mutahiwa kutoka Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Bwana Salehe Songoro Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Songoro, na wafanyakazi wa Kampuni ya Songoro na
wale wa TEMESA.
Akiongea baada ya zoezi hilo, Dkt.
Mgwatu amesema wakazi wa Mwanza wana kila sababu ya kujivunia kuanza
kwa ujenzi wa kivuko hicho kwani kitakapokamilika kitasaidia kurahisisha
usafiri wa abiria na mali zao na hivyo kuimarisha uchumi wao. Aidha Dk.
Mgwatu amemtaka Mkandarasi kuhakikisha anamaliza kujenga kivuko ndani
ya muda uliopangwa kwenye mkataba na kuzingatia ubora wa hali ya juu.
Pia ameishukuru Serikali kwa kuendelea kutenga fedha za maendeleo kwa
ajili ya miradi ya vivuko kwa lengo la kuboresha huduma za usafiri. Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Songoro ameahidi kukamilisha mradi
huo kwa wakati huku akisisitiza kuwa kampuni yake imejipanga vyema
kufanya kazi kwa kasi kwa kuwa malighafi kwa ajili ya ujenzi wa kivuko
tayari ipo kwenye eneo la ujenzi.
Kivuko hicho kipya
kitakapokamilika kitafanya idadi ya vivuko vinavyotoa huduma katika eneo
la Kigongo Busisi kufikia vinne vikiwemo vile vya MV. Sengerema, MV.
Misungwi, pamoja na MV. Sabasaba.
0 comments:
Post a Comment