Mkuu wa Kikosi cha Jeshi la Kujenga
Taifa (JKT) namba 831 KJ Mgulani, Luteni Kanali, Zacharia Godfrey
Kitani, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu
askari wa kikosi hicho kujitolea damu na kufanya usafi katika maeneo
mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya
maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho nchini kote.
Jengo la Utawala la Hospitali hiyo.
Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa
Hospitali hiyo, Bilal Babu akimtoa damu, Kijana wa JKT, Damiani
Ambross wakati akichangia damu.
Vijana wa JKT, wakisubiri kuchangia damu.
Vijana wa JKT wakisukuma mkokoteni wenye matofari wakati wakifanya usafi katika hospitali hiyo.
Vijana wa JKT wakiweka matofari katika eneo maalumu
Usafi ukiendelea kufanywa.
Mti ukikatwa.
Matawi ya mti yakikatwa tayari kwa kuondolewa
Usafi ukiendelea.
Hapa ni kazi tu ya usafi.
Mti uliokatwa ukisukumwa tayari kwa kuondolewa katika
eneo hilo.
Mti uliokatwa ukiondolewa eneo la tukio.
Askari hao wa JKT wakiondoa matawi ya mti yaliyokatwa.
Takataka zikiondolewa hospitali hapo kwa kutumia mifuko maalumu.
Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa
Hospitali hiyo, Hassan Mwage akimtoa damu, Kijana wa JKT, Kafumu
Godfrey Ambross wakati akichangia damu.
Mtaalamu wa Sayansi ya Maabara wa
Hospitali hiyo, Heri Shekighenda akimtoa damu, Kijana wa JKT, Kafumu
Godfrey Ambross wakati akichangia damu.
Vijana wa JKT wakijisajili majina yao kabla ya kutoa damu kwaajili ya kuchangia.
Takataka zikiondolewa.
Na Dotto Mwaibale
ASKARI wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)
Kikosi namba 831 KJ Mgulani, wamejitolea kuchangia damu pamoja na
kufanya usafi katika maeneo mbalimbali ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe
Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho
nchini kote.
Akizungumza na waandishi wa habari Dar
es Salaam leo, Mkuu wa Kikosi hicho Luteni Kanali Zacharia Godfrey
Kitani alisema kila maadhimisho hayo yanapofanyika wamekuwa wakifanya
shughuli za kijamii kama kufanya usafi na mwaka huu wameona wafanye
usafi na kuchangia damu katika hospitali hiyo ili kusaidia wananchi.
“Ni kawaida yetu katika kuadhimisha siku
ya kuanzishwa jeshi letu sisi kama askari kushiriki shughuli mbalimbali
za kijamii katika maerneo tofauti tofauti kwa siku kadhaa leo hii
tunafanya usafi katika Hospitali ya Temeke na kutoa damu na tutaendelea
katika maeneo mengine hadi siku ya kilele cha maadhimisho haya hapo
kesho ” alisema Kitani.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo,
Husna Msangi alisema msaada huo wa damu waliochangia askari hao
utasaidia kwa kiasi kikubwa kukabiliana na changamoto ya damu
hospitalini hapo kutokana kuwa na mahitahi makubwa ya damu kwa wagonjwa.
Alisema mahitaji ya damu katika
hospitali hiyo ni makubwa hivyo amewaomba wadau wengine wajitokeze
kuchangia damu ili kuokoa maisha ya watu ambao wataweza kupoteza maisha
kwa kukosa damu.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
0 comments:
Post a Comment