HOSPITALI ya Taifa Muhimbili (MNH) imefunga
mashine 30 za ki-elektroniki katika maeneo ya kutolea huduma kwa lengo la kuimairisha
na kudhibiti ukusanyaji wa mapato.
Akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili, Profesa
Lawrence Museru amesema mfumo huo utawezesha kuokoa zaidi ya Sh milioni 300.
Amesema Muhimbili imefunga mashine hizo kwa
kushirikiana na Kampuni ya Maxcom na kwamba huduma hiyo itasaidia kuokoa muda wa mgonjwa wakati wa kulipia
huduma za matibabu.
“Muhimbili tunahudumia wagonjwa zaidi ya
2000 kwa siku, tulianza kudhibiti ukusanyaji wa mapato kwa kushirikiana na
benki ya NMB tukaweza kuokoa takriban Sh milioni 300 lakini bado kuna baadhi ya
malipo yalikuwa yakifanyika kwa ‘cash’.
“Kwa kuanzisha mfumo huu wa malipo ya kadi
kwa kushirikiana na Maxcom kuanzia sasa hakuna malipo yatakayofanyika kwa
‘cash’,”.
Mkurugenzi wa Fedha na Mipango Muhimbili,
Gerald Jeremiah amesema mfumo huo umefanyiwa majaribio tangu Julai 10, mwaka
huu hadi Agosti 15, mwaka huu na umeonesha mafanikio makubwa.
Mkururugenzi wa Kampuni ya Maxcom barani
Afrika, Jameson Kasati alisema mteja ataweza kulipia huduma kwa njia
mbalimbali.
“Mfumo huu unatumia njia mbili ambazo ni kadi
na mfumo wa malipo kwa njia ya simu (mobile money), tumeanza na M-pesa, Airtel
na Tigo baadae tutakwenda kwenye mitandao mingine,” alisema.
Amesema ili kuongeza mtaji wake, kampuni
hiyo tayari imepeleka ombi katika Mamlaka ya Mitaji na Hisa ili waweze kununua
hisa kwenye kampuni hiyo.
MWISHO.
0 comments:
Post a Comment