Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imegoma kupokea bangi inayodaiwa kukutwa nyumbani kwa Mlimbwende Wema Sepetu, kama kielelezo.
Hakimu
Mkazi Mkuu, Thomas Simba ametoa uamuzi huo leo Agosti 31, kutokana na
hoja za kupinga kupokelewa zilizowasilishwa na Wakili wa Wema, Tundu
Lissu.
Awali
Shahidi wa kwanza katika kesi hiyo, Mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu
wa Serikali, Elias Mulima akiongozwa na Wakili wa Serikali, Costantine
Kakula aliomba kutoa bangi kama kielelezo katika kesi hiyo mahakamani
ambayo alidai kupima msokoto mmoja na vipisi viwili vinavyodaiwa kukutwa
nyumbani kwa Wema na kugundua ni bangi.
Mulima
aliomba kuitoa bahasha iliyofungwa, yenye muhuri, saini ya shahidi huyo
na namba ya maabara 291 ya 2017 mahakamani hapo kwa utambuzi.
Wakili
Lissu alipinga kisipokelewe kama kielelezo cha ushahidi kwa sababu
ndani ya bahasha hiyo kuna vitu zaidi ya msokoto mmoja na vipisi viwili
vinavyodaiwa kuwa ni bangi.
“Mheshimiwa
hakimu vipisi viwili vyenye majani ukiviangalia kwa makini ni vishungi
vya sigara ambayo imetumika kwa sababu vina alama ya kuungua, kwetu
vinaitwa twagooso, kitu kinachoitwa msokoto wa bangi hakijulikani
kimefungwa fungwa tu karatasi, kuna kibiriti, karatasi nyekundu,
haiwezekani vitu vilivyotolewa kwenye bahasha kuwa ndiyo vitu shahidi
alivielezea, mahakama isikubali kuvipokea kama kielelezo,” alidai Lissu.
Baada
ya mahakama kugoma kupokea kielelezo hicho imepanga kuendelea
kusikiliza ushahidi wa Jamhuri Septemba 12 na 13 mwaka huu. Wema na
wenzake wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia dawa za kulevya.
0 comments:
Post a Comment