MHE HAMAD ASIFU TEKNOLOJIA YA SERIKALI MTANDAO KATIKA KILIMO
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid Muhammed Akisikiliza kwa makini maelezo mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Serikali ya Mtandao wakati alipotembelea Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid Muhammed Akisikiliza kwa makini maelezo mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Serikali ya Mtandao Kutoka kwa Bi Caroline Munuo Marealle Mtaalamu wa Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) wakati alipotembelea Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid Muhammed Akisikiliza kwa makini maelezo mbalimbali kuhusu Teknolojia ya Serikali ya Mtandao wakati alipotembelea Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid Muhammed Akisikiliza kwa makini maelezo mbalimbali kuhusu Sera na Mipango wakati alipotembelea Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Na Mathias Canal, Lindi
Wizara ya kilimo Mifugo na Uvuvi imepongezwa kwa kusimamia utekelezaji wa mkakati wa serikali mtandao ndani ya wizara ambao utawezesha matumizi ya teknolojia katika kutoa huduma za serikali zinazohusiana na kilimo
Jambo hilo litawezesha kuboresha huduma, kupanua upatikanaji wa huduma kwa wahitaji ndani ya sekta lakini hata na nje ya sekta ya kilimo na vile vile kujaribu kuwa wabunifu wa kujua na kutoa huduma wanayohitaji wadau wa kilimo.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid Muhammed wakati alipotembelea Maonesho ya Kilimo (Nanenane) yanayofanyika katika viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mhe Hamad alisema kuwa malengo makubwa ya vizara ni kutoa huduma bora za kilimo, kuweka mazingira bora kwa wazalishaji na kuchangia kikamilifu ukamilishaji na tija katika kilimo, kusimamia na kuwezesha ushirika kutoa huduma bora na zenye tija kwa wateja.
Wizara ya Kilimo kupitia kitengo cha Teknolojia, Habari na Mawasiliano (TEHAMA) tayari kimesimika Video Conference ya kisasa inayofanya kazi kurahisisha mawasiliano baina ya kilimo makao makuu Dodoma na Ofisi za kilimo Dar es salaam.
Hata hivyo kitengo hicho kinaendelea na usimikaji wa mfumo wa Taifa wa Taarifa za kilimo (National Agricultural Information System NAMIS) ambao utakuwa kitovu cha taarifa za kilimo kwa wadau wote wa kilimo Tanzania.
Sambamba na hayo pia uwekaji wa mtandao kuunganisha wizara nzima upo katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na uunganishi wa mtandao wa kompyuta uliopo uliopo katika makao makuu ya Wizara na kwenye vituo vya utafiti.
MWISHO
0 comments:
Post a Comment