Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akimkabidhi fulana na kofia Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kushoto) zitakazotumika wakati wa kilele wa Maadhimisho ya Siku na Nane Nane kitaifa mjini Lindi.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akimkabidhi fulana na kofia Mkuu wa
Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kushoto) zitakazotumika wakati
wa kilele wa Maadhimisho ya Siku na Nane Nane kitaifa mjini Lindi.
Na Mwandishi wetu,
Katika
kudhirisha umuhimu wa Siku ya Nane Nane Benki ya Maendeleo ya Kilimo
Tanzania (TADB) imeunga mkono kwa kutoa fulana na kofia zitakazovaliwa
katika siku ya kilele cha maadhimisho hayo.
Akizungumza
wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa
Wageni Maalumu uliopo katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi, Mkuu wa
Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema kuwa TADB imeonesha
mfano kwa taasisi nyingine nchi kwa kutambua umuhimu wa Nane Nane
inayofanyika kitaifa mkoani humo.
“Tunaishukuru sana TADB kwa mchango huu ambao kwa hakika utang’arisha maadhimisho yetu,” alisema.
Bw.
Zambi aliongeza kuwa mchango huo unachagiza kauli mbiu ya Maonesho hayo
isemayo “Zalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia
uchumi wa kati”.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga
amesema kuwa Benki ya Kilimo imeunga mkono Maonesho hayo ya Nane Nane
kwa kutambua umuhimu wa kilimo na kutimiza malengo ya Benki hiyo
katika kusaidia kilimo nchini.
“Mchango
huu unasadifu malengo ya kuanzishwa kwa TADB ambayo yanajumuisha
Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni
endelevu nchini Tanzania; na Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya
Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema Bw. Assenga.
Maadhimisho
ya maenesho hayo yatafikia kilele siku ya tarehe 08 ambapo Mgeni rasmi
wa anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.
0 comments:
Post a Comment