METDO Tanzania

METDO Tanzania

Wednesday, August 30, 2017

MAFUNZO YA PS3 YAENDELEA MKOANI DODOMA

01
Mwezeshaji kutoka Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma (PS3) Christopher Masaaka ambaye pia ni Afisa Uchumi  kutoka Halmashauri ya Wangingómbe Mkoa wa Njombe akitoa mafunzo kwa moja ya kundi la washiriki wa mafunzo ya Mfumo wa Kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo Mjini Dodoma. Kushoto ni Wagisha Ronald na Hussein Kiranga (Katikati) kutoka Taasisi ya GIZ-TGPSH.
02
Baadhi ya Maafisa Uchumi, Mipango na Makatibu Afya kutoka Manispaa ya Singida wakijadili jambo wakati wa mafunzo ya Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa leo Mjini Dodoma.
03
Baadhi ya Watumishi mbalimbali wakiwemo Maafisa Uchumi, Mipango na Makatibu Afya kutoka Halmashauri za Mkoa wa Manyara wakifuatilia mafunzo ya Mfumo wa kielektroniki (PlanRep) iliyoboreshwa wa kuandaa Mipango, Bajeti na Ripoti za Mamlaka ya Serikali za Mitaa yanayoratibiwa na Mradi wa Uimarishaji Sekta za Umma (PS3) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) leo Mjini Dodoma.

(Picha na Beatrice Lyimo-MAELEZO
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com