METDO Tanzania

METDO Tanzania

Thursday, July 13, 2017

DED MNASI: WANANCHI WA ILEJE WATANUFAIKA NA ARDHI YAO

 Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Ileje Haji Mnasi akiwa Na baadhi ya wananchi wa kijiji Shinji
Mkurugenzi wa Ileje Haji Mnasi akibadilishana mawazo na baadhi ya wananchi wa kijiji cha Shinji
 
Na fredy Mgunda, Ileje

Wananchi wa Halmashauri ya Ileje Mkoani Songwe kunufaika na maeneneo yaliyotengwa  kwa ajili ya vikundi vya wajasiliamali na Vijana ikiwa ni kuendelea kutekeleza ilani ya chama cha mapindizi chini ya Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr John pombe Magufuli.

Akizungumza wakati wa utowaji elimu na urasimishaji wa maeneo ya vikundi vya vijana vijijini Mkurugenzi wa Halmamashauri hiyo ndugu Haji Mnasi alisema nia ya uongozi wa halimashauri hiyo ni kuhakikisha wananchi wake wananufaika kiuchumi kupitia rasilimali zilizopo katika Wilaya hiyo ikiwemo Ardhi, amesema wananchi wengi wanamiliki Ardhi lakini wanashindwa kuzitumia kupata mikopo kutokana na kutozirasimisha 

Mkurugenzi huyo akiwa pamoja na Watendaji wake (Maafisa Ardhi,Maendeleo ya Jamii na afisa ushirika, wamewatebelea  wananchi vijijini  ili kutoa Elimu ya Uwekezaji na Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi katika Wilaya ya Ileje.

Pia Mnasi alisema Lengo la ziara hiyo akiawa na wataalam wa kada hizo ilikuwa ni Kuhakikisha kuwa halmashauri inawezesha Urasimishaji na Uwezeshaji wa Wananchi kiuchumi kwa kupitia Vyama vya Ushirika na Vikundi vya kiuchumi na kijamii Vilivyo sajiliwa ndani ya Halmashauri ya Wilaya. 

Ziara hii ya vijijini imewezesha mambo yafatayo kufanyika:

1. Kubaini maeneo yaliyo tengwa na Vikundi vyenyewe au Serikali ya kijiji kwa ajili ya Shughuli za Vikundi hivyo. 

2. Kurasimisha Maeneo yaliyobainishwa kwa ajili ya shughuli za Kikundi cha Mpozile katika kijiji  cha Msia, Kikundi cha Umoja katika kijiji cha Shinji yamebainishwa, kupimwa na yako katika mchakato wa kutwaa hati miliki ya maeneo hayo na Vijana SACCOS ya Yuli katika kijiji cha Yuli 

Mkurugenzi huyo wa Ileje Mkoani Songwe alisema watahakikisha eanashirikiana na wananchi kwa kwenda vijijini bila kuwasubilia wao kufika ofisini, bali kuwafuata na kutatua changamoto  ili kuendana Na kasi ya Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania katika kutekeleza Sera ya  chamaa cha mapinduzi CCM.

Afisa ardhi  Daniel Mpagama na afisa maendeleo vijana na uwekezaji David Gunzar walimpongeza Mkurugenzi huyo kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuleta maendeleo katika wilaya ya Ileje na kuwaomba wafanyakazi wengine kuunga mkono ili kufikia malengo.

Naye mwenyekiti wa kijiji cha Shinji Daudi Kanyika alisema kuwa hajawahi kumuona Mkurugenzi kama huyo kwa kuwa wakurugenzi wengi huwa wanashinda maofisini tu ila Mkurugenzi Mnasi amefika hadi huku kijijini na kutufungulia fursa za kimaendeleo
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com