Naibu
Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk.
Hamisi Kigwangalla (MB),mapema leo Agosti 17,2017 amefanya ziara ya
kutembelea vituo mbalimbali vya Afya na kujionea utendaji kazi katika
sekta hiyo Mkoani hapa.
Dk.Kigwangalla
ametembelea Kituo cha Afya Kaloleni, kituo cha Afya Levolosi, kituo
cha Afya Ngarenaro, Kituo cha Afya Daraja Mbili, Kituo cha afya Mkonoo
na Kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya .
Akizungumza
wakati wa kutoa maagizo kwenye vituo hivyo amemuagiza Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Arusha Dk. V.Timothi Wonanji na Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri
ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe na viongozi wengine wa mkoa akiwemo
kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi kuhakikisha
wanatatua changamoto za Afya ikiwemo ukosefu wa vyumba vya upasuaji na
ukosefu wa vitendanishi katika mashine za vipimo vya maabara.
"Mnavyo
vituo vya Afya 7. Mnahitaji kuwekeza zaidi ili mnunue vifaa vya Maabara
na kufanyia ukarabati hivyo vilivyopo. Kuna vifaa vya maabara vya
kisasa ambavyo ni ‘portable’ na havina gharana kubwa. Tunataka mtenge
fedha za kutosha ili kuimarisha sekta ya Afya" aliagiza Dk Kigwangalla.
Aidha
akitoa agizo wakati kukagua kituo cha Afya Daraja Mbili ameagiza mara
moja jengo la Chumba cha Upasuaji cha kituo hicho kianze kazi ndani ya
wiki mbili na upasuaji ufanyike ikiwemo wataalamu kuwapo hapo muda
wote.
"Naagiza
ndani ya wiki mbili. Huduma za upasuaji zifanyike hapa kwani mnacho
kila kitu , vifaa vingi na vya kutosha na jengo zuri la kisasa"
alisema, Dk Kigwangalla.
Katika
hatua nyingine Dk.Kigwangalla ameagiza kituo cha Afya Kaloleni
kuhakikisha wanajenga wodi ya akina mama na kukamilisha maboresho ya
Chumba cha upasuaji.
"Hiki
kituo hakina hadhi ya kuwa Kituo cha Afya. Ni sawa na Zahanati tu
maana kama hakuna huduma muhimu za upasuaji na wodi ya wazazi, nahitaji
kuona munakamilisha mara moja" alieleza Dk. kigwangalla.
Katika
hatua nyingine, Dk. Kigwangalla ameweza kukagua sehemu za Maabara, wodi
za wazazi na vyumba vya upasuaji pamoja na maeneo mbalimbali ya
hospitali kuona utendaji wa kazi muhimu na namna ya utoaji wa huduma
zinazotolea katika Jiji la Arusha.
Mbali
na kukagua vituo hivyo vya Arusha, Dk. Kigwangalla pia ameweza
kutembelea baadhi ya maeneo yanayotarajiwa kujengwa vituo vya Afya
kwenye maeneo hayo ya Wilaya ya Arusha.
Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa Kituo cha Afya Kaloleni namna watakavyojenga wodi ya Wazazi katika moja ya maeneo ndani ya kituo hicho cha Afya Kaloleni, Wilaya ya Arusha, mapema leo Agosti 17,2017 wakati wa ziara ya kikazi ya kutembelea vituo mbalimbali vya Afya na kujionea utendaji kazi katika sekta hiyo ya Afya Mkoani hapa.
Naibu Waziri wa Afya, Maemdeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dk. Hamisi Kigwangalla (MB), akitoa maelezo kwa uongozi wa kituo cha Afya Levolosi juu ya uwekaji wa vifaa vya Maabara hiyo
Dk. Kigwangalla akkagua chumba cha upasuaji katika kituo cha Afya Levolosi
Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro
Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro
Dk. Kigwangalla akikatisha mitaa kwa miguu akitokea kituo cha Afya Levolosi wakati akielekea kukagua kituo cha Afya cha Ngarenaro. Kulia kwake ni Mganga Mkuu wa Mkoa wa Arusha Dk. V. Timothi Wonanji na kushoto ni Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya ambacho kinajengwa cha Muriet Mpya wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akiwa katika kituo cha Afya Themi wakati wa ziara yake hiyo. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Rebecca Mongi
Dk. Kigwangalla akikagua kituo cha Afya kinachojengwa wakati wa ziara yake hiyo.
Dk. Kigwangalla akipata picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa sekta ya Afya Jiji la Arusha wakati wa ziara yake hiyo.
Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya jiji la Arusha Dk. Baraka Mundhe akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla wakati alipotembelea kituo cha Afya Kaloleni.
Dk. Kigwangalla akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati akizungumza na waandishi wa habari
Dk. Kigwangalla akitoa maagizo kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Bi. Rebecca Mongi wakati wa ziara yake hiyo ya kukagua vituo vya Afya
0 comments:
Post a Comment