METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, August 5, 2017

Benki ya NMB yachangia Milioni 10 Tamasha la Usalama Barabarani

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Serikali wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akikabidhi sehemu ya jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) zilizotolewa na NMB kuchangia Tamasha la Usalama barabarani linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika hafla fupi ya kupokea jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 zilizotolewa na Benki ya NMB zikiwa na jumbe mbalimbali kuhamasisha uzingatiaji sheria na kanuni za usalama barabarani kuchangia Tamasha la Usalama barabarani linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017. Kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Serikali wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo. Kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Serikali wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akikabidhi sehemu ya jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) zilizotolewa na NMB kuchangia Tamasha la Usalama barabarani linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017 katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,

BENKI ya NMB leo imekabidhi mchango wa jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 zikiwa na jumbe mbalimbali kuhamasisha uzingatiaji sheria na kanuni za usalama barabarani ikiwa ni kuchangia kufanikisha Tamasha kubwa la Usalama barabarani linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa hapo baadaye.

Msaada huo umekabidhiwa leo jijini Dar es Salaam kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni na kuipongeza Benki ya NMB pamoja na wadhamini wengine kwa kujitoa kuchangia tamasha hilo la Usalama Barabarani lenye kauli mbiu “Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi Milele” litakalofanyika Agosti 12, 2017.

Akikabidhi msaada huo, Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na Serikali, Omari Mtiga alisema NMB linaunga mkono usalama wa raia na mali zao na ndio maana limevutiwa kuchangia ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo limelenga kutoa elimu kwa umma juu ya uzingatiaji wa sheria na kanuni za usalama barabarani.

Mtiga alisema NMB imekuwa mshirika mkubwa wa Jeshi la Polisi Tanzania kwani imekuwa ikishirikiana kuunga mkono juhudi mbalimbali za jeshi katika kulinda usalama wa raia na mali zao. Alisema NMB itaendelea kushirikiana na Jeshi hilo ili kuhakikisha wananchi ambao ni wateja wake wanakuwa salama salimini pamoja na mali zao.

Kwa upande wake, Naibu Waziri Masauni alisema tamasha hilo lililopangwa kufanyika Uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017 na kushirikisha michezo na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii na mapambano ya mpira wa miguu linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

Michezo itakayofanyika ni pamoja na mpira wa miguu kati ya Jeshi la Polisi na Bodaboda, Wabunge na Wasanii wa Bongo Movie na Wasanii wa Bongo Fleva. Tamasha hilo kwa ujumla litakuwa likitoa elimu ya masuala mbalimbali ya usalama barabarani lengo likiwa kupambana na ajali za barabarani.
Baadhi ya wasanii wakiwa katika mkutano huo.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika hafla fupi ya kupokea jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 zilizotolewa na Benki ya NMB zikiwa na jumbe mbalimbali kuhamasisha uzingatiaji sheria na kanuni za usalama barabarani kuchangia Tamasha la Usalama barabarani linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017.
Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com