Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na
Serikali wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akikabidhi sehemu ya
jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 kwa Naibu Waziri
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
zilizotolewa na NMB kuchangia Tamasha la Usalama barabarani
linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017 katika Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika hafla fupi ya kupokea
jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 zilizotolewa na
Benki ya NMB zikiwa na jumbe mbalimbali kuhamasisha uzingatiaji sheria
na kanuni za usalama barabarani kuchangia Tamasha la Usalama barabarani
linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017. Kulia ni
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, SACP Fortunatus Musilimu.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na
Serikali wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akizungumza katika hafla
hiyo. Kulia ni Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Wadogo na
Serikali wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto) akikabidhi sehemu ya
jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 kwa Naibu Waziri
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia)
zilizotolewa na NMB kuchangia Tamasha la Usalama barabarani
linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017 katika Uwanja wa
Taifa, jijini Dar es Salaam.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
BENKI ya NMB leo imekabidhi mchango wa
jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 zikiwa na jumbe
mbalimbali kuhamasisha uzingatiaji sheria na kanuni za usalama
barabarani ikiwa ni kuchangia kufanikisha Tamasha kubwa la Usalama
barabarani linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa hapo baadaye.
Msaada huo umekabidhiwa leo jijini Dar
es Salaam kwa Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi
Hamad Masauni na kuipongeza Benki ya NMB pamoja na wadhamini wengine kwa
kujitoa kuchangia tamasha hilo la Usalama Barabarani lenye kauli mbiu
“Hatutaki Ajali, Tunataka Kuishi Milele” litakalofanyika Agosti 12,
2017.
Akikabidhi msaada huo, Mkuu wa Kitengo
cha Wateja Wadogo na Serikali, Omari Mtiga alisema NMB linaunga mkono
usalama wa raia na mali zao na ndio maana limevutiwa kuchangia
ufanikishaji wa tamasha hilo ambalo limelenga kutoa elimu kwa umma juu
ya uzingatiaji wa sheria na kanuni za usalama barabarani.
Mtiga alisema NMB imekuwa mshirika
mkubwa wa Jeshi la Polisi Tanzania kwani imekuwa ikishirikiana kuunga
mkono juhudi mbalimbali za jeshi katika kulinda usalama wa raia na mali
zao. Alisema NMB itaendelea kushirikiana na Jeshi hilo ili kuhakikisha
wananchi ambao ni wateja wake wanakuwa salama salimini pamoja na mali
zao.
Kwa upande wake, Naibu Waziri Masauni
alisema tamasha hilo lililopangwa kufanyika Uwanja wa Taifa Agosti 12,
2017 na kushirikisha michezo na burudani mbalimbali kutoka kwa wasanii
na mapambano ya mpira wa miguu linatarajiwa kufunguliwa na Rais wa
Tanzania, John Pombe Magufuli.
Michezo itakayofanyika ni pamoja na
mpira wa miguu kati ya Jeshi la Polisi na Bodaboda, Wabunge na Wasanii
wa Bongo Movie na Wasanii wa Bongo Fleva. Tamasha hilo kwa ujumla
litakuwa likitoa elimu ya masuala mbalimbali ya usalama barabarani lengo
likiwa kupambana na ajali za barabarani.
Baadhi ya wasanii wakiwa katika mkutano huo.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza katika hafla fupi ya kupokea
jezi za mpira wa miguu seti 10 pamoja na fulana 500 zilizotolewa na
Benki ya NMB zikiwa na jumbe mbalimbali kuhamasisha uzingatiaji sheria
na kanuni za usalama barabarani kuchangia Tamasha la Usalama barabarani
linalotarajia kufanyika uwanja wa Taifa Agosti 12, 2017.
No comments:
Post a Comment