Na Mwandishi Wetu, Kasulu
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umewataka Vijana wenzao wa Kenya kushiriki uchaguzi mkuu wa Agosti 8 mwaka huu katka muweka madarakni Rais wa nchi hiyo bila kughiibiwa, kushawishiwa na kuiingizwa katika vitendo vya machafuko , umwagaji wa damu au kuzuka mapigano.
Aidha umoja huo umetoa wito kwa vijana wote wa Afrika Mashariki wakatae kutumiwa na wanasiasa wanaotumia ukabila, udini au ukanda kinyume na nguvu za maamuzi ya wengi.
Ushauri huo umetolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka alipozumgumza na makundi ya vijana, wanachama wa CCM na jumuiya zake katika ukumbi wa CCM wilaya Buhingwe Mkoani hapa .
Shaka alisema UVCCM ingependa kuwaona vijanawa kenya wakishiriki uchaguzi mkuu wao kwa kujali na kutunza amani, utulivu na usalama ili kulinda misingi ya mshikamano na umoja wa kitaifa nchi humo.
Alisema Vijana EA iwe mwiko na kejeli kwao kubabaishwa na wanasiasa wenye mitazamo hasi ya kutaka kuvuruga amani, uchonganishi na kuwatumia vijana kwa manufaa yao hatimaye amani kutoweka.
"Machafuko na umwagaji damu ukitokea nchi yoyote EAC utaigharimu nchi nyingine, yatazalisha wakimbizi, yataathiri miasha ya vijana, yatawapa dhiki watoto ,wanawake na wazee. Hatutaki EA liwe eneo la machafuko na uchonganishi "Alisema Shaka.
Shaka alisema Afrika Mashariki inahitaji kujenga nguvu ya umoja , upendo na kuendeleza ushirikiano utakaowapa nafasi vijana wa nchi moja kwenda nchi nyingine ili kutafuta maisha kwa njia za kisheria bila kujiingiza katika wizi na uhalifu
Aidha aliwataka vijana katika maeneo ya pembezoni mwa mkoa wa kigoma, vijijini na mijini katika wilaya saba za mkoa huo kutojihusisha na ujangili, uhalifu au kutumia silaha au vitendo kiharamia.
Kaimu Katibu Mkuu alisema nchi yetu ina ardhi ya kutosha kwa kuendeleza shughuli za Uvuvi, biashara halali na kujiingiza katika ujasiriamali zitakazoinua vipato kiuchumi
"Kijana wa Tanzania kipi kinamfanya aibe, awe jambazi, mhalifu anayetumia silaha na kupora mali wakati fursa za kufanya kazi vijana zipo na huzitumii "Alieleza .
Vile vile Shaka aliponda tabia za uvivu, kukata tamaa na vijana kutamani maisha mazuri bila kujituma na kufanya kazi huku akisema tamaa hizo huwa chanzo cha kushiriki ujambazi na uporaji.
Hata hivyo kiongozi huyo wa UVCCM aliwasisitiza vijana mkaoni hapa kuendelea kuiunga mkono ccm kwa kuwa ndiyo chama pekee cha siasa kinachotetea maslahi ya vijana na chenye mipango na mikakati ya kuwainua kimaisha .
Katika mkutano huo jumla ya wanachama wapya 200 toka CUF ,Chadema, ACT Wazalendo na NCCR -Mageui walihamia CCM na kukabidhiwa kadi mpya za uanachama .
Shaka anaendelea na ziara yake ya kikazi akizungumza na wanachama wa ccm katika mikutano ya ndani ambapo kesho ataelekea wilaya ya kibondo mkoani humu .
0 comments:
Post a Comment