METDO Tanzania

METDO Tanzania

Saturday, July 29, 2017

MBUNGE WA ILEMELA MGENI RASMI MIAKA 25 YA SHALLOM CARE

Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula leo ameshiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 25 tangu kuanzishwa kwa kituo cha kupambana na kudhibiti maambukizi ya  Virusi vya Ugonjwa wa Ukimwi kinachomilikiwa na Jimbo Kuu la Katoliki Jijini Mwanza

Akizungumza katika sherehe za maadhimisho hayo Dkt Angeline Mabula ameitaka Jamii kuungana kwa pamoja katika kuendeleza mapambano dhidi ya ugonjwa huo huku akiasa kuachwa kwa unyanyapaa na kujinyanyapaa kwa watu wenye Virusi vya ugonjwa wa Ukimwi  sambamba na kuzitaka asasi zote zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya Ugonjwa huo kuacha kutegemea zaidi misaada kutoka nje ya nchi na badala yake zianze kufikiria njia mpya na bora ya kujisimamia katika kutekeleza shughuli zake

‘… Niwashukuru sana wafadhili kwa namna walivyokuwa wakitusaidia  katika kutoa huduma bora kwa watu wetu lakini niziombe asasi zetu kuanza kufikiria njia mpya na bora  katika kujiendesha kwasababu bila hivyo tutaendelea siku zote kusubiri kukinga mikono kuliepuka hilo niitake jamii kukiona kituo hiki ni cha kwetu, tukione kituo hiki ni msaada kwa jamii nzima kwa hiyo tunaowajibu pale wanapoleta kilio chao wakiomba msaada basi tuwasaidie ili tuweze kusimama pamoja sisi wenyewe …’ Alisema

Aidha Mbunge huyo mbali na kulishukuru kanisa kwa kuunga mkono Serikali katika kutekeleza shughuli mbalimbali za kijamii amewahakikishia kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika binafsi katika kuhakikisha vita dhidi ya maambukizi mapya ya ugonjwa wa Ukimwi inafanikiwa na kuwapa  kompyuta mbili  ili kurahisisha utendaji wao wa kazi

Akimkaribisha mgeni rasmi mwakilishi wa mkuu wa mkoa Mwanza ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Nyamagana Mhe Marry Tesha mbali na kukipongeza kituo hicho kwa kufikisha miaka 25 amemwagiza mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela John Wanga kuhakikisha anaanda mpango mkakati wa kuvisaidia vituo vyote  vinavyotekeleza shughuli zenye tija kwa jamii ili kuisaidia Serikali katika kutimiza malengo yake ya kuwasaidia wananchi wake

Akihitimisha sherehe hizo Baba Askofu Jimbo Kuu Katoliki Mkoa wa Mwanza Mhashamu Thaddaeus Ruwa'chi mbali na kuishukuru Serikali chini ya Rais Mhe John Magufuli kwa kuunga mkono shughuli zinazotekelezwa na asasi binafsi likiwemo Kanisa Katoliki  ameomba kupatiwa usajili wa kuwa kituo cha kutolea huduma majumbani (CTC) ili kurahisha upatikanaji wa huduma kwa walengwa

‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane kuijenga ’

Imetolewa na
Ofisi ya Mbunge
Jimbo la Ilemela
29.07.2017

Share:

0 comments:

Post a Comment

Copyright © WAZO HURU | Powered by Blogger Design by ronangelo | Blogger Theme by NewBloggerThemes.com