Waziri Mkuu akisalimiana na viongozi mbalimbali wakati alipowasili katika Shule ya Msingi ya Uhuru Mchanganyiko Dar es Salaam jana
Mshereheshaji akiongoza uzinduzi huo
Katibu Tawala wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo (kulia) akizungumza jambo na maofisa wa Jeshi la Magereza kabla ya kuwazili mgeni rasmi
Afisa Elimu Ilala, Elizabeth Thomas (kulia) akiwaunga mkono wanafunzi hao kwakutoa burudani kwa kucheza nao
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Umoja iliyopo Yombo Kiwalani ikitumbuiza wimbo wa Makirikiri katika uzinduzi huo, ambapo Waziri, Ndalichako ametowa ofa wafike Dodoma kuendeleza kutowa huduma hiyo katika sherehe zinazo tarajiwa kufanyika mjini humo hivi karibuni
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akihutubia katika uzinduzi huo
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akitowa salam za mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati wa uzinduzi na ugawaji na usambaza wa vifaa kwa wanafunzi wenye uhitaji maalum Nchi nzima uzinduzi uliyofanyika Dar es Salaam jana, ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Wanahabari wakiwa kazini
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa uzinduzi huo, ambapo alianza kuwashukuru walimu na kuwasihi kwa namna wanavyo shirikana ilikuweza kulifikisha gurudumu la Elimu mahala tunapohitaji lifike,
Hayo aliyasema jana Jijini Dar es Salaam katika uzinduzi wa vifaa maalumu kwa wanafunzi wenye mahitaji hayo ambapo alisisitiza na kuwashukuru waandaaji na kumpa heshima ya kumualika kuwa mgeni rasmi.
Aidha kipekee kabisa nishukuru Shirika la Lanes lililoshirikiana na Serikali yetu kusaidia upatikanaji wa vifaa hivi ambapo punde nitazindua na kufikabidhi ugawaji wa vifaa hivi.
Kwaniaba ya Serikali napenda kuwaahidi kwamba vifaa hivi vitatumika kama vilivyo kusudiwana vitawafikia walengwa wote tayari kwa matumizi
Ndugu wananchi, Walimu na Wanafunzi, nitazindua zoezi la usambazaji vifaa kwa ajili ya wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwa mikoa yote 26 ya Tanzania Bara
Zoezi la hili hapa lilitanguliwa na zoezi la usambazaji wa vifaa vya masomo ya Sayansi, kwenye Sekondari, tulifanya Lugalo kwa hiyo ni siku ya Elimu na sasa tumefika hapa katika Shule ya Msingi ambapo tutahitimisha zoezi hili
Zoezi hili litanufaisha shule za Msingi 213 kati ya shule 408 na shule za Sekondari 22 kati ya shule 45 zenye wanafuzi wenye mahitaji maalumu pamoja na wanafunzi wasioona na wenye uwezo wa usikivu hafifu, Serikali pia imenunua vifaa kwa ajili ya walimu kufundishia na vifaa hivyo ilivitumike katika kufundishia na kwaajili ya upimaji wa elimu ya mwanafunzi, aliendelea kusema waziri Mkuu
Hiki ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya ya Rais Wetu mpendwa Dkt, John Pombe Joseph Magufuli ya kuhakikisha kila mtoto wa kitanzania mwenye umuri wa kwenda shule anapata huduma hiyo bila ya kujali hali hiyo
Vifaa vinavyo sambazwa vitasaidia kukuza kiwango cha taaluma kwenye shulezetu zenye wanafunzi wenye mahitaji maalumu na vilevile vitaongeza hamasa kwa watoto kupata elimu, alisema waziri Mkuu
Natowa wito na kuwasihi wazazi wote nchini tusikate tamaa na wala tusikatishwe tamaa ili tutimize ndoto za watoto wetuza kufika mahali wanapokusudia , jambo hili linawezekana kwa vijana hawa kupata elimu na wala tusiwafiche na Mh, Waziri hapa amesisitiza kwamba watoto hawa wasifichwe katika manyumba
Nivizuri kutambua watoto wenye mahitaji maalumu ili liweze kuwa endelevu na kwa Serikali hii inadhamira ya Dhati kutekeleza mahitaji ya wanafunzi hao
Serikali imedhamiria kuongeza maslahi kwa walimu na kudhamiria kutwapa mafunzo ya mara kwa mara kuendana na mitaala , nakuendelea kusema
Wizara ichukue hatua stahiki na kwawale wazazi wanao waficha watoto majumbani na wakibainika wazazi hao bazi hatua kali zichukuliwe juu ya mza au wazazi. Mtoto akisha zaliwa siwako ni wataifa zima na nijukumu la Serikali kumuwekea mpango endelevu na kwahiyo agizo hili litekelezwe
Pia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametowa wito kusimami nidhamu kwenye eneo letu la elimu ili tujenge Taifa la wasomi na kwa yeyote atakaye bainika kuharibu mwenendo wa mtoto wakike na aka mpa ujauzito mwanafunzi na ikibainika atakwenda jela miaka 30, awe mzazi kumuozesha mwanafunzi ati mnataka ,ng'ombe, mbuzi ,kondoo na ikibaanika jela miaka 30, au kumtorosha na kumpeleka chumbani kwako ni miaka 30, kuowa mwanafunzi miaka 30,Serikali imedhamiria kuwekeza katika kumlinda mtoto wa kike. sasa nitowe shukrani zangu kwa za dhati wote waliojiltolea katika kukamilisha hafla hii na kuwashukuru Ilala na kuwaona vijana wa hamasa
Pia Benk ya Duni, na wadau wote na viongozi wa elimu na kumshukuru Mkuu wa Shule hii . Sasa nakwenda kuzindua rasmi
0 comments:
Post a Comment