Asanteni wote kwa mjadala huu unaonihusu.
Kwa wanaounga mkono, asanteni, tusaidianeni kupata majibu ya changamoto za maendeleoyetu, siku moja tutajua maana ya kila kitu.
Kwa wanaopinga ninawashukuru kwa somo mahiri kabisa: Dada Ananilea, Mtatiro, Innocenti, etal...ninawaelewa, siwaombi mnielewe, kwa maana kuelewa ni bora kuliko kueleweka.
Kwa walioko kwenye siasa za nchi hii tunajua wote kuwa kipindi hiki na vipindivilivyopita wote tunatekeleza ilani ya chama kinachoongoza nchi. Mengine ni maoni mbadala. bajeti ni hiyo na mipango ni hiyo. Bunge pamoja na mijadala yote linapitisha mapendekezo ya CCM. Wapinzani wanajadili kioo cha CCM.
Nilimpa Rais mteule (wakati ule) ilani ya chama changu. Leo amenipa yake. Nimeipokea na nitaisimamia kwa sababu ndiyo inayoongoza kwa sasa. tukiisoma ilani hiyo tutakuta ina mambo yote yaliyomo kwenye vision 2025. hakuna zaidi ya hii kwa Tanzania isipokuwa ya ACT 2015 ambayo iliongeza vionjo vya tafiti na takwimu. Mengine yanafanana na matamanio ya ziada ya 2025. Ya Chadema / CUF pia haina tofauti.
Kanuni moja ya maisha ni kuenenda kulingana na uzoefu ulioupata, kwa sababu uzoefu ni uhalisia. Sifikiri kama ukuu wa mkoa ni cheo cha kujisifia zaidi ya huduma yake kwa wananchi.Nikiweza kutoa huduma hii nitamshukuru sana Mungu. Ninaomba anijalie hilo. mengine kila mtu atajibu kwa kadiri ya yanayomtoka si yanayomwingia.
Mimi ni Kiongozi wa kisiasa. Nimepewa nafasi ya Kisiasa. Si cheo cha Kisiasa. Ndivyo ninavyoamini.
Anna
0 comments:
Post a Comment